Hivi karibuni kumekuwa na hili ongezeko la wanaoitwa wasaliti katika vyama vya siasa.Tumeshuhudia wakishughulikiwa kwa namna tofauti.Napenda kuamini katiba imeheshimiwa na haki ya kujitetea imetumika. Ingawa hukumu siku zote hauwezi kuwa kitu kizuri wakati mwingine ni lazima,nachojaribu kutafakari na kukosa majibu ni sababu ya kuwepo kwa usaliti wenyewe.Ni tamaa?Ni kurubuniwa? Au itikadi za vyama hazieleweki?Na sasa tunapaswa kufanya nini ili kuondokana na hii tabia ya kuwa ndege mchana,popo usiku.