Kimsingi nimesukumwa kutoka ndani kuanzisha uzi huu, kwa kila mtanzania hii itamhusu, tujifunze kuipenda serikali yetu na nchi yetu kiujumla. Sina maana ya kuwagawa kivyama au kiitikadi isipokuwa NAOMBA KILA MTANZANIA UNAEMFAHAMU MTU AMBAE NI POTENTIAL KWA TAIFA LETU yaani kama unajua mtu aliyegundua kitu chchte mfano, aliyegundua na kutengeneza engine ya pikipiki au chochote, au mtu aliyebuni chchte ambaye anastahili kuendelezwa.
Naomba tuwaorodheshe humu kwa majina yao na namba zao za simu na kazi zao (walicho kitengeneza) ili kuisaidia serikali kulifanyia kazi jambo hili. Maana imeonekana tuna Wataalam wengi Tanzania ambao bado hatuna watumia.
Napenda kuwasilisha watu wa Serikali kama mkiona hii ina tija naomba muifikishe kwa Mh. Rais na tutafutane, nitakuwa huru kuwapa ushirikiano juu ya hili.
TANZANIA TUNAWEZA KUWA NA VIWANDA TUKIJITATHMINI WENYEWE KWANZA."INAWEZEKANA"
Karibuni kwa hoja