Habari wadau,
Hii ni rasmi kwa nchi jirani kwa bunge la nchi hiyo kupitisha sheria inayowataka raia wote wa nchi hiyo na wageni watakao penda kuoa binti toka Malawi ni sheria kuoa binti wa nchi hiyo ni lazima awe amefikisha umri wa miaka 18.
Chini ya hapo utashitakiwa na jamuhuri kuoa mtoto na kifungo chake si chini ya miaka 30 jela.
Moja ya sababu ya kuidhinisha sheria hiyo ni sababu ya vifo vingi vya mabinti walio olewa chini ya umri ikiambatana na pia husababisha kujifungua watoto njiti, kushindwa kulea familia, mimba kutoka, kufariki kwa watoto wakati wa kujifungua, wengi wao kujifungua kwa upasuaji sababu ya nyonga.
Hivyo kuanzia kesho sheria hiyo itaanza kazi rasmi.
Niushauri kwa bunge na watunga sheria walichukue kama inafahamika kuwa na maamuzi ya kupiga kura nikuanzia miaka 18 chini ya hapo ni mtoto nasi tufuate kulinda haki za watoto.