Tunaupongeza uongozi wa Mhe Magufuli kwa kulivalia njuga suala la rushwa ndani ya Kamati za Bunge. Kuna kesi ya Mbunge aliyetuhumiwa na rushwa katika awamu ya nne lakini mwisho wa siku alikuja kushinda kesi kwa mazingira ambayo sisi wananchi mpaka sasa hatujaelewa.
Halmashauri wanapata sana matatizo kuhusiana na ripoti zao wanapopeleka mbele ya Waheshimiwa Wabunge. Hapa kuna mizengwe sana. Pili, hata mahesabu yao yanayopelekwa kwa CAG kuna shida sana. Mpaka Halmashauri ije ipate UNQUALIFIED OPINION kuna kazi.
Ninakuomba, wewe una vijana wako, hebu wafanye utafiti ni mataizo gani Halmashauri zinazopata katika ukaguzi wa mahesabu yao na kuja kupata OPINION kwa kila Halmashauri. Pili, ni matatizo gani Halmahauri wanazopata wakati wakiwasilisha mahesabu yao mbele ya Waheshimiwa Wabunge. T
afiti hizi zitakupa picha kamili kitu gani kinaendelea na itakusaidia mahali pa kuanzia ili kurekebisha matatizo yaliyoonekana.