Matanga
JF-Expert Member
- Nov 13, 2019
- 2,281
- 3,974
SIMBA WATUHUMIWA KUTAKA KUMUHONGA KADO
Waandishi Wetu, Dar na Morogoro
MSHAMBULIAJI wa zamani wa Simba, Ulimboka Mwakingwe amekamatwa na polisi mkoani Morogoro akihusishwa na njama za kuhujumu mchezo wa Ligi Kuu baina ya Simba na Mtibwa uliopangwa kufanyika leo kwenye Uwanja wa Jamhuri.Mshambuliaji huyo aliyetemwa na mabingwa hao wa soka wa Tanzania Bara msimu uliopita alikamatwa juzi na kuachiwa kwa dhamana jana asubuhi baada ya kuhojiwa na polisi wa kituo cha Manungu.
Habari ambazo Mwananchi imezipata zinaeleza kuwa Ulimboka alikamatwa akiwa na Sh400,000 na alipohojiwa alidai kuwa alikuwa akienda kumlipa deni kipa wa Mtibwa Sugar, Shaaban Kado.
Polisi walithibitisha kukamatwa kwa mchezaji huyo wa zamani wa kimataifa, lakini wakasema uchunguzi dhidi ya tuhuma hizo unaendelea.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Thobias Andengenye aliliambia Mwananchi jana kuwa uongozi wa Mtibwa wilayani Mvomero ulimfikisha Ulimboka kituo cha polisi kwa tuhuma za kutaka kutoa hongo ya Sh400,000 kwa Kado ili acheze chini ya kiwango kwenye mechi ya leo.
"Ni Kweli tumepokea taarifa hizo kuwa Ulimboka alifikishwa kituoni Mtibwa baada ya kujaribu kumpa Kado fedha kiasi hicho ili aachie mabao katika mchezo wao wa kesho [leo] dhidi ya Simba," alisema Kamanda Andingenye.
‘’Hata hivyo, Ulimboka amekana kuwa hakutaka kumrubuni kipa huyo na kusema ni kweli alikwenda Mtibwa akiwa na kiasi hicho cha fedha kwa lengo la kumlipa deni mchezaji huyo kwa sababu (Kado) ni rafiki yake ndani na nje ya mpira.
"Alitwambia kwamba anachofahamu katika siku za nyuma yeye alimwazima Kado kiasi hicho cha fedha na alifika Mtibwa kwa kuwa wakati huo ulikuwa muda sahihi wa kwenda kumlipa kwa kuhofia kuwa kama angechelewa, angeweza kumuudhi."
Kado amekuwa mmoja wa wachezaji nyota walioibukia katika siku za karibuni na alionyesha kiwango cha juu wakati Taifa Stars ilipolazimisha sare ya bao 1-1 na Algeria mjini Blida.
Kipa huyo anatarajiwa kusimama langoni Oktoba 9 wakati Stars itakapoikaribisha Morocco kwenye mechi ya pili ya michuano ya kuwania tiketi ya kucheza fainali za Mataifa ya Afrika za mwaka 2012.
Taarifa kutoka ndani ya uongozi wa Mtibwa Sugar ziliarifu Mwananchi jana kuwa walipokea taarifa kutoka kwa Kado akieleza kuwa Ulimboka alikuwa akitaka kumpatia fedha ili aiachie Simba katika mchezo wa leo na ndipo wao wakamshauri ampe muda ili wafike mahali (Manungu) wakiwa na polisi na ndivyo alivyofanya.
Alipoulizwa kuhusu suala hilo, afisa habari wa klabu ya Simba, Clifford Ndimbo alikana klabu yake kuhusika na tuhuma hizo na kudai kuwa kuna watu wanataka kuwavuruga ili wafanye vibaya katika mchezo huo.
''Sisi hatuhusiki na tuhuma hizo... kwanza Ulimboka aliondoka Simba kwa ugomvi, iweje leo uongozi wetu umtume atoe rushwa? Habari si za kweli,'' alisema Ndimbo.
Lakini tangu habari hizo zilipofumuka jana asubuhi wadau mbalimbali wa Simba, wakiwemo waandishi watano wa habari za michezo walikuwa wakipiga simu kujaribu kushawishi habari hiyo isichapishwe na Mwananchi kwa madai kuwa itashusha heshima ya klabu hiyo.
Tukio hilo limetokea wakati Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) likiwa limetangaza kuwafungia waamuzi wanne kwa makosa ya kuvurunda mechi walizochezesha za Ligi Kuu Bara zinazoihusisha Simba, Yanga, Azam na Kagera. Klabu za Azam na Arusha FC ziliwahi kulalamikia uamuzi wa mechi zao dhidi ya Simba na Yanga zikidai uamuzi ulilenga kuzibeba timu hizo kongwe nchini.
Hongahonga Fc
Sent using Jamii Forums mobile app