Tufanye M23 wangekuwa nchi nyingine ukubwa wao ungekuwa upi?

ndege JOHN

JF-Expert Member
Aug 5, 2015
21,368
50,738
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) ambayo ukubwa wake ni takriban sawa na Ulaya Magharibi, ni nchi kubwa katika eneo la Jangwa la Sahara.

DR Congo imejaliwa kuwa na maliasili za kipekee, ikiwa ni pamoja na madini kama vile kobalti na shaba, uwezo wa uzalishaji umeme kwa maji, ardhi kubwa ya kilimo, na yenye msitu wa pili kwa ukubwa duniani.

Hata hivyo kwa bahati mbaya, watu wengi nchini DRC hawajanufaika na utajiri huu.

Historia ndefu ya uwepo kwa makundi ya waasi tofauti tofauti nchini humo kumesababisha migogoro, misukosuko ya kisiasa na ukosefu wa utulivu kuwa chanzo cha matatizo mengi yanayokabili raia.

Lakini ndani ya DRC, kuna makundi zaidi ya 100 ya waasi wenye silaha na yanajiendesha kwa kutumia rasilimali za taifa hilo.

Fahamu baadhi ya makundi ya waasi ambayo yamekuwa yakitatiza shughuli za kawaida nchi humo.

Allied Democratic Forces - ADF

Hili ni kundi lenye silaha linalofanya kazi mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC).

Wapiganaji wa ADF kimsingi wanatoka Uganda na DRC, huku baadhi yao wakiripotiwa kutoka nchi nyingine za Afrika Mashariki.

Kundi hilo la Kiislamu liliundwa miaka ya 1990 na mara nyingi lilihusika na mizozo ya ndani na taifa la Uganda baada ya kuchukua silaha dhidi ya rais wa muda mrefu nchini Uganda Yoweri Museveni likidai kuwa serikali ilikuwa inaendesha mateso dhidi ya Waislamu.

Baada ya kushindwa na jeshi la Uganda mwaka 2001 lilihamia mkoa wa Kivu Kaskazini nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo.

Hata hivyo, kundi la ADF liliibuka tena mwaka 2014 kwa kendesha misururu ya mashambulizi dhidi ya raia nchini DRC na shughuli zake zimechukua mkondo wa kundi la jihadi huku mashambulizi yake mengi yakidaiwa kutekekelezwa kwa jina la kundi la Islamic State (IS).

Musa Seka Baluku akawa kiongozi wa kundi hilo mwaka 2015 kufuatia kukamatwa kwa mtangulizi wake Jamil Mukulu huku Bakulu akiripotiwa kutangaza kulitii kundi la IS mwaka 2016.

M23 ni kundi lililotokana na Chama cha Kitaifa cha Ulinzi wa Watu, National Congress for the Defence of the People – CNDP.

Kilitokana na Watutsi wa Congo na jumuiya nyingine za makabila katika Kivu ya kaskazini na kusini wakidai kuwa wanabaguliwa.

Kikundi hiki cha waasi kiliwahi kupigana na serikali ya DRC kati ya 2006 na 2009.

Serikali ya DRC kisha ikaendesha harakati za kuwapokonya silaha lakini baadaye harakati hizo zikasitishwa.
Waasi wa M23 wanachukuliwa kuwa wa asili ya Rwanda na wanajulikana kama “Rwandophones”.

Wapiganaji hao walijipa jina la M23 baada ya mkataba wa amani wa Machi 23, 2009 uliotiwa saini na serikali na wanamgambo wa zamani wanaounga mkono Watutsi.

Wapiganaji wengi wa waasi wa M23 wanatoka jimbo la Kivu Kaskazini na haswa kutoka Masisi na Rutshuru.
Maeneo haya yako karibu na mpaka wa Rwanda ambako mapigano hutokea mara kwa mara.

M23 wanahusishwa na mapigano yanayoendelea kipindi hiki wakikabiliana na wanajeshi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ambapo zaidi ya watu 100,000 wametoroka makazi yao na makumi ya wengine kuuawa.

Rwanda, imeshutumiwa kwa kuwaunga mkono waasi wa M23 na matokeo yake ikaishia kufurushwa kwa balozi wake nchini DR Congo.

Hata hivyo, Rwanda imekanusha madai hayo.

kuachiwa jeshi la taifa pekee.

APCLS inajiweka kama adui mkali wa M23, na CNDP kabla ya hapo, haya ni makundi ambayo uungwaji mkono wake kutoka Rwanda (na Uganda) umerekodiwa kwa wingi.

Wengine wanawaita wasiotaka mabadiliko na baadhi ya makamanda wa APCLS wamekataa maelewano yoyote na maadui zao katika mazungumzo mbalimbali ya mchakato wa amani.

APCLS imedumisha uhusiano mzuri na kundi la waasi la FDLR kwa miaka mingi.

Maï Maï Sheka (Nduma Defence of Congo - NDC)
Kamanda wa kundi hili la waasi ni Ntabo Ntaberi Sheka katika Wilaya ya Walikale ya Kivu Kaskazini, Mashariki mwa Congo.

Ntabo Ntaberi Sheka alijiunga na Jenerali wa zamani wa CNDP Bosco Ntaganda tangu katikati ya 2011.

Mnamo Julai 2011, Umoja wa Mataifa ulichapisha ripoti ya kina iliyoangazia kuhusu ubakaji wa takriban watu 387 - kati ya Julai 30 na Agosti 2, 2010, katika vijiji 13 kando ya barabara ya Kibua hadi Mpofi katika eneo la Walikale, kulingana na Tovuti ya Human Rights Watch.

Ripoti ya Umoja wa Mataifa ilisema Mai Mai Sheka alikuwa miongoni mwa muungano wa makundi matatu yenye silaha yaliyohusika na ubakaji wa halaiki, na kumtaja Sheka kama mmoja wa viongozi waliobeba jukumu la kamandi.

Wachunguzi wa Umoja wa Mataifa waligundua kwamba Sheka na viongozi wengine wawili wa vikundi vyenye silaha walikuwa wakifahamu vyema mipango na mpangilio ya operesheni... iliyofanyika.

Ilikuwa ni moja ya kesi kubwa zaidi zilizorekodiwa za ubakaji wa watu wengi mashariki mwa Congo katika miaka ya hivi karibuni.

Mai Mai Raïa Mutomboki
Raia Mutomboki, ni kundi la waasi lililoanzishwa mwaka wa 2005 katika Wilaya ya Shabunda ya Kivu Kusini na mwasi wa jeshi la Congo Mchungaji Jean Musumbu ili kukabiliana na mauaji ya FDLR.

Kundi hilo linajumuisha vikundi mbalimbali vinavyoongozwa na viongozi wa mitaa na waasi wa FARDC.

Inasemekana kwamba lilibadilika kutoka kwa wanamgambo wa kiparokia na kuwa kundi la vurugu lililosambazwa katika sehemu kubwa za Kivu Kaskazini na Kusini huku kukiwa na dosari katika mikataba mbalimbali ya amani mashariki mwa DRC.

[Wanafanya kazi] kwa misingi ya wanamgambo wa kujilinda ambao wamejaribu kukabiliana na tishio la FDLR vilivyo, ikiwa ni pamoja na [kupitia] ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu kama vile mauaji ya kiholela.

Aidha, mwaka 2012 ripoti ya Umoja wa Wamataifa ilimshtumu Jenerali Gabriel Amisi kwa kuendesha mtandao wa kusambaza silaha kwa wawindaji haramu pamoja na makundi ya waasi ikiwemo kundi hilo la Mai Mai Raia Mutomboki.
Chanzo BBC SWAHILI
 

Attachments

  • efb24620-6f9d-11ed-94b2-efbc7109d3dd.jpg.jpeg
    efb24620-6f9d-11ed-94b2-efbc7109d3dd.jpg.jpeg
    102.9 KB · Views: 8
  • b524f480-6f9d-11ed-94b2-efbc7109d3dd.jpg.jpeg
    b524f480-6f9d-11ed-94b2-efbc7109d3dd.jpg.jpeg
    32.9 KB · Views: 7
  • 2db26cd0-6f9d-11ed-94b2-efbc7109d3dd.jpg.jpeg
    2db26cd0-6f9d-11ed-94b2-efbc7109d3dd.jpg.jpeg
    76.2 KB · Views: 9
  • 70bc4a50-6f9d-11ed-94b2-efbc7109d3dd.jpg.jpeg
    70bc4a50-6f9d-11ed-94b2-efbc7109d3dd.jpg.jpeg
    56.1 KB · Views: 11
Back
Top Bottom