TUCTA mko wapi wafanyakazi tunadhalilishwa?

mamba1

JF-Expert Member
Jun 24, 2015
466
248
Chama cha wafanyakazi nchini Tanzania kiko kimya juu ya manyanyaso wanayofanyiwa wafanyakazi. Manyanyaso yamekuwa mengi miongoni mwa hayo ni;
1.Makato ya bodi ya mikopo kupanda kutoka 8% mpaka 15%.

2.Kuzuia wafanyakazi kupanda vyeo mpaka wapitie kozi maalum. Na hizo kozi huenda
zikatolewa kwenye vyuo ambapo ada yaweza kuwa millions of money.

3.Kupandishwa kwa PAYE kutoka 9% mpaka 15. Hili litamgusa kila mfanyakazi.

Hivi mnataka tupokee 2000 kila mwisho wa mwezi tuoneeni huruma wafanyakazi kwani viongozi wetu wako kwenye usingizi wa pono.

[HASHTAG]#Msalimieni[/HASHTAG] bashite viongozi wetu.
 
Sidhani kama hiki chama kipo kwa ajili ya kulinda maslahi ya wanachama wake. Ni kama wanapokea maagizo kutoka kwa watawala. Chama gani kinaona wanachama wake wanafukuzwa kazi bila utaratibu huku wengine wakiwekwa maabusu kinyume na utsratibu.

Hawa viongozi wetu hawarifai na ni wakati sasa tumuombe Tundu Lisu aje kugombea uongozi na huku kwa maana hawa waliyopo wameshindwa na wanamuogopa Baba bashite.
 
Sio haki mods kuuhamisha uzi wangu kwenye forum nyingine pia kazi ni siasa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…