Tuambiane ukweli: Suala sio dawa za kulevya, ni kujenga hofu kwa kuonyesha nguzu za serikali

Synthesizer

Platinum Member
Feb 15, 2010
12,415
22,026
Nimefikiri sana juu ya hili, nikaona kwamba ni kama kulikuwa na kampeni fulani ya serikali kutaka kuonyesha inaweza kukamata mtu yeyote na kumweka ndani bila hata kujali nafasi yake katika jamii au sheria za nchi. Nahisi lengo lilikuwa kutia hofu wananchi, na suala la madawa ya kulevya lilitumika kama daraja tu, a means to an end.

Naona watu kama Mbowe, Gwijama na Manji na wasanii maarufu ilikuwa wawe kielelezo, ili mlalahoi kama wewe na mimi tuone kwamba kama hawa watu wanaweza kuwekwa ndani kirahisi namna hiyo, basi sie wananchi wa kawaida je?

Na tukumbuke kwamba tukio hili limeenda sambamba na Raisi Magufuli kuwakumbusha wakuu wa JWTZ na Polisi kwamba lazima watu wayaogope majeshi yao. Katumia neno kuheshimu - kwani watanzania hawawaheshimu Polisi na JWTZ? Heshima gani raisi anataka wananchi wawe nayo - woga?

Mie nadhani huu ni mkakati wa kutia hofu ndani ya wananchi ili tuwe taifa la kutodiriki kukosoa.
 
Is true
 
Kwan lini tuliacha kuyaogopa? Au tunalalamika hela ngumu kwan zaman hela ilikua nyepes,,,
 
Mkuu wewe ni Msukuma? Hapo kwenye "NGUZU" ndo umeniacha hoi!!
 
Mleta shauri uko sahihi kabisa, Yaani iwe kama ilivyo kuwa Libya au kama zilivyo nchi za Burundi,Rwanda na Uganda.
 
Kama ilivyokuwa Libya na ilivyo kwa Burundi, Rwanda na Uganda ndiyo tunaelekea uko tena kwa speed ya ajabu sana, mkuu wa nchi anakosa ushirikiano ndani ya CCM hana budi kivitumia vyombo vya dola na baadhi ya wateule wake.
 
kama suala sio madawa ya kulevya basi endelea kuuza unga,au kama ulikuwa huuzi basi anza sasa.
 
Sure! Naisi kama yanatengenezwa mazingira kuna jambo kubwa litakuja kutokea ukombeleni kamasio muda wa kukalia kiti sijui
 
Sure, mikakati ya uongozi, waliambiwa kila Mara lazima msikike. Baada ya episode hii kufungwa inakuja nyingine
 
Kama suala ni madawa ya kulevya serikali ingefunga viwanda vyote vya pombe. Nayo inalevya.
 
kama suala sio madawa ya kulevya basi endelea kuuza unga,au kama ulikuwa huuzi basi anza sasa.
Unaelewa maana ya dawa za kulevya kutumika kama daraja? Kiingereza tunasema leverage. Haina naana dawa za kulevya zitumike, inachomaanisha ni kwamba biashara hapa ilikuwa kutia hofu ila bidgaa ikaunganishwa na dawa za kulevya. Hizo ni mbinu kama ukitaka kuuza sukari lazina mteja anunue na najani ya chai.

Inabidi uwe kipofu sana kutoona kwamba serikali ina mkakati mkubwa wa kutia watu hofu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…