Tuacheni kujitetea kwa kutokujua Kiingereza. Tukubali kuwajibika

GoldDhahabu

JF-Expert Member
Apr 29, 2023
4,968
6,742
Kwenye Biblia, Adam alipoulizwa kwa nini kala tunda alilokatazwa, alijitetea kuwa si kosa lake, bali kashawishiwa na mke wake. Ingelikuwaje kama angelikubali kosa na kuomba msamaha?

Daudi alipofahamu kuwa kagundulika kuwa alimwua Huria baada ya kuzini na mke wake, hakujitetea kuwa ni mke wa Huria ndiye aliyezembea kwa kuoga kwenye bafu lisilo na paa kulikopekekea yeye kumwona na kumtamani, bali alilikubali kosa lake na kuwa tayari kuwajibika kwa makosa yake. Kulikiri kosa lake kulimfanya asamehewe.

Ni kanuni iliyothibitishwa kuwa huwezi kukibadili usichokikabili.

Huwezi kurekebisha kosa ambalo unaamini kuwa umesababishiwa na mtu au kitu chochote. Ni mpaka kukubali kuwajibika kwa asilimia mia moja ndipo utakapoona njia ya kutokea.

Kwa nchi za Afrika Mashariki, hasa Tanzania, Kenya, Rwanda na Uganda, inafahamika kuwa ni Watanzania ndiyo wanaoongoza kwa Kiingereza cha kiubabaishi.

Ingawa tuna lugha yetu adhimu ya Kiswahili, lakini si kizuizi cha kuielewa na English ambayo kimsingi, ndiyo lugha ya Kimataifa kwa sasa. Kwa nini tusikijue kwa ufasaha na huku:

1. Ndiyo lugha ya kufundishia kuanzia Sekondari hadi Chuo Kikuu

2. Ni kati ya "official languages" katika taasisi za uma.

Mtu pekee mwenye uhalali wa kutokukijua ni ambaye hajapitia Sekondari, lakini kwa wengineo wote, ni "uzembe", na mpaka mtu akubali kuwa ni uzembe wake ndiyo atachukua hatua. Miaka minne mtu aliyokaa Sekondari ingemtosha kukijua Kiingereza fasaha, hata kama hatamfikia Kiranga na Nyani Ngabu.

Kuwa na lugha ya Kiswahili isiwe kikwazo. "English" ndiyo lugha inayoongoza duniani kwa kuwa na waongeaji wengi. Inakadiriwa kuwa na watumiaji bilioni moja na nusu.

Kwa wale ambao Kingereza kilitupiga chenga tulipokuwa masomoni, tusione haya kuchukua hatua za makusudi kujinoa katika uwezo wa kuimudu 'English". Ukiwekeza masaa mawili kwa siku, baada ya miezi sita, hutakuwa kama ulivyo sasa(kama hukijui kwa ufasaha kwa sasa).

Kujitetea hakutusaidii. Tukubali kuwa tulizembea, na tujisahihishe, huku tukivisaidia vizazi vijavyo visirudie makosa yetu.
 
Tukiimarishe Kiswahili ili kufikia 2050 kiwe lugha mojawapo kubwa na mashuhuri duniani.
 
Nani atakayefanya hivyo?

Mpaka sasa, kwa mujibu wa takwimu, haimo miongoni mwa lugha 20 zinazozungumzwa sana duniani.

Ni muhimu kukikuza Kiswahili, lakini tukiwa tunakimudu vyema Kiswahili na Kiingereza, tunakuwa tumejiweka mahali pazuri kuzifaidi fursa mbalimbali duniani.

Itapendeza tukiwa tunamudu vizuri lugha tatu:
1. Kiswahili
2. Kilugha (lugha ya asili)
3. English
 
Huwezi kuwa rubani kama hujui kingereza kuanzia level 3. Hata kama una master ya physics na maths
 
Unaikokotoaje hiyo mkuu? Nataka nijue kama nimeshavuka level 1 ama safari bado ndefu!
 
Kwenye hiyo taaluma wana level za kingereza unapaswa kujua ili upewe leseni ya kurusha ndege. Ni lazima sio ombi, na level 5 ni ile kingereza unaongea fluently kama cha mzaliwa wa pale london katikati.
 
Kwenye Biblia, Adam alipoulizwa kwa nini kala tunda alilokatazwa, alijitetea kuwa si kosa lake, bali kashawishiwa na mke wake. Ingelikuwaje kama angelikubali kosa na kuomba msamaha?

Daudi alipofahamu kuwa kagundulika kuwa alimwua Huria baada ya kuzini na mke wake, hakujitetea kuwa ni mke wa Huria ndiye aliyezembea kwa kuoga kwenye bafu lisilo na paa kulikopekekea yeye kumwona na kumtamani, bali alilikubali kosa lake na kuwa tayari kuwajibika kwa makosa yake. Kulikiri kosa lake kulimfanya asamehewe.

Ni kanuni iliyothibitishwa kuwa huwezi kukibadili usichokikabili.

Huwezi kurekebisha kosa ambalo unaamini kuwa umesababishiwa na mtu au kitu chochote. Ni mpaka kukubali kuwajibika kwa asilimia mia moja ndipo utakapoona njia ya kutokea.

Kwa nchi za Afrika Mashariki, hasa Tanzania, Kenya, Rwanda na Uganda, inafahamika kuwa ni Watanzania ndiyo wanaoongoza kwa Kiingereza cha kiubabaishi.

Ingawa tuna lugha yetu adhimu ya Kiswahili, lakini si kizuizi cha kuielewa na English ambayo kimsingi, ndiyo lugha ya Kimataifa kwa sasa. Kwa nini tusikijue kwa ufasaha na huku:

1. Ndiyo lugha ya kufundishia kuanzia Sekondari hadi Chuo Kikuu

2. Ni kati ya "official languages" katika taasisi za uma.

Mtu pekee mwenye uhalali wa kutokukijua ni ambaye hajapitia Sekondari, lakini kwa wengineo wote, ni "uzembe", na mpaka mtu akubali kuwa ni uzembe wake ndiyo atachukua hatua. Miaka minne mtu aliyokaa Sekondari ingemtosha kukijua Kiingereza fasaha, hata kama hatamfikia Kiranga na Nyani Ngabu.

Kuwa na lugha ya Kiswahili isiwe kikwazo. "English" ndiyo lugha inayoongoza duniani kwa kuwa na waongeaji wengi. Inakadiriwa kuwa na watumiaji bilioni moja na nusu.

Kwa wale ambao Kingereza kilitupiga chenga tulipokuwa masomoni, tusione haya kuchukua hatua za makusudi kujinoa katika uwezo wa kuimudu 'English". Ukiwekeza masaa mawili kwa siku, baada ya miezi sita, hutakuwa kama ulivyo sasa(kama hukijui kwa ufasaha kwa sasa).

Kujitetea hakutusaidii. Tukubali kuwa tulizembea, na tujisahihishe, huku tukivisaidia vizazi vijavyo visirudie makosa yetu.
Lugha yakiswahili haijtoshelezi hivyo haifai kuwa lugha ya kufundishia...mfano mdogo tu
Nitajie rangi za bendera ya Taifa Kwa kiswahili..Nina Imani utakosa...
 
English" ndiyo lugha inayoongoza duniani kwa kuwa na waongeaji wengi. Inakadiriwa kuwa na watumiaji bilioni moja na nusu.
Mimi nilikua najua Chinese Mandarin ndio lugha inayoongoza duniani kuwa na waongeaji wengi kumbe ni mambo yamebadilika.
 
Lugha yakiswahili haijtoshelezi hivyo haifai kuwa lugha ya kufundishia...mfano mdogo tu
Nitajie rangi za bendera ya Taifa Kwa kiswahili..Nina Imani utakosa...
Hiyo ni rahisi sana mkuu: buluu/bluu (blue), nyeusi (black), kijani (green), na njano (yellow).
 
Mimi nilikua najua Chinese Mandarin ndio lugha inayoongoza duniani kuwa na waongeaji wengi kumbe ni mambo yamebadilika.
Chinese Mandarin ni ya pili kuzungumzwa for both native and non natives speakers, ila kwa native speakers, Chinese Mandarin inashika nafasi ya kwanza.

Kwa msingi huo, kama utazingatia native speakers pekee, lugha zinazoongoza kwa kuwa na watumiaji wengi ni Mandarin Chinese, ikifuatiwa na Spanish, kisha English, then Hindi.

Lakini ikiwa utajumuisha natives and non natives, ya kwanza ni English ikifuatiwa na Chinese Mandarin.
 
Kwenye hiyo taaluma wana level za kingereza unapaswa kujua ili upewe leseni ya kurusha ndege. Ni lazima sio ombi, na level 5 ni ile kingereza unaongea fluently kama cha mzaliwa wa pale london katikati.
Nitajuaje level yangu?

Naweza kujipima mwenyewe?

Nitajisikia vibaya sana nikiambiwa bado nipo level 1😄, ila nipo tayari kujiendeleza nipande levels.
 
Don't follow follow me without because. You can't me am another.
🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣

Nimelazimika kusoma mara kadhaa ndipo nikaielewa.

Hata mhadhiri wa English toka Cambridge University hataelewa ulichomaanisha
 
Kwenye hiyo taaluma wana level za kingereza unapaswa kujua ili upewe leseni ya kurusha ndege. Ni lazima sio ombi, na level 5 ni ile kingereza unaongea fluently kama cha mzaliwa wa pale london katikati.
Ubarikiwe kwa kunijulisha juu ya uwepo wa level 5.

Nimegundua bado sijaiva. Acha nijitutumue kuanzia sasa kwa msaada wa YouTube, halafu baada ya miezi miwili, niende mahali fulani kujipima.
 
Back
Top Bottom