KERO TTCL ni sikio la kufa! Haiwezekani kwa zaidi ya miezi sita nimeomba huduma ya fiber nyumbani wananizungusha tu

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Habari za muda huu Wanajamvi,

Hii Kampuni ya TTCL ni sikio la kufa na wala halisikii dawa tena, haifanyi vizuri kwenye mawasiliano ya simu kawaida wala kwenye Internet. Mimi nipo Dar es Salaam na nimeomba huduma ya kufungiwa internet nyumbani (fiber) na sasa yapata miezi sita ila sijafungiwa wala hakuna kitu cha maana kinachoeleweka kutoka kwao.

Ukihitaji Internet wanasema inabidi uombe kupitia website yao na ukifanya hivyo kwa kweli ni kwa haraka tu maombi yako yanapokelewa na kuambiwa yanafanyiwa kazi. Unataarifiwa mara moja kwa ujumbe mfupi (sms) na hapo hapo kwenye website yaani unaweza kusema kweli hawa jamaa ni top-notch na nitapata huduma fasta kabisa.

Ila hapo sasa ndio mchezo unapoanza, utazungushwa hadi ujute mwenyewe. Nimepiga simu zaidi ya mara 5 kwenye namba yao ya huduma kwa wateja wanapokea na jibu lao mara zote linakuwa "Ni kweli umeomba fiber, ombi lako tunaliona na tunalifanyia kazi. Mafundi wetu wa eneo lako watakupigia simu ili waje kukuunganishia". Baada ya hapo nimekuwa nikuliza kwamba hao mafundi watakuja lini atleast mnipe muda kabisa nijue au nifanye taratibu nyingine, hapo utajibiwa "Tafadhali kuwa mvumilivu, mafundi wetu watakutafuta"

Hata hivyo, baadhi ya watu wanasema TTCL hawaji kufunga internet hadi wapate shinikizo kutoka kwa Wakubwa zao. Yaani utafungiwa Internet ukiwa unawajua hao wakubwa ambapo hili ni jambo la ajabu kabisa kwa Taasisi ya Serikali kama ile inayoendeshwa kwa kodi za Wananchi.

TTCL kwa sasa sitaki tena huduma yenu hii, nitafunga internet ya watu wengine na kwa mtindo huu hamtakuja kuwa shirika la maana na hata nashangaa lile gawio mnatoa kwa Serikali huwa mnatoa wapi. Hii Kampuni inakufa hata Wakurugenzi wabadilishe kwa namna gani.

Pia soma;
1. Kuchelewa kupatikana kwa huduma ya internet ( fiber) TTCL

2. Huduma ya TTCL ya kutoa Internet nyumbani ni mbovu sana
 
Binafsi nina zaidi ya mwaka mmoja toka niombe hii huduma na sijapata. Swali ambalo hawataki kulisikia ni kuwauliza lini utapata huduma.

Wanapenda wakupe majibu ya jumla jumla ili ujiondokee zako wao wasubiri mwisho wa mwezi msg ya muamala wa mshahara iingie.

Halafu wanapenda kutangaza kweli hii huduma ya fiber mlangoni utadhani wapo serious vile.
 
We unasema Miezi 6?

Si wengine tuna miaka mitatu tangu ile siku ya kwanza wanazindua kampeni yao ya fiber mlangoni watu tulianza process na mpaka sasa hakuna responding.

Huko ofisini kwao tumeenda sana mpaka ikafika hatua tukaanza hadi kuwajua wafanyakazi wa pale kwa majina.

Ikafika muda unaingia tu ofisini unaskia "Aah Scars naona umekuja kufuatilia swala lako" na mimi najibu "ndio Edward si unajua bwana Omary siku ile alinisisitizia kuwa leo nikija nitamkuta Mateo ambaye anahusika na eneo langu"
 
Yani ilifikia hivyo, kwa waliokuwa wageni waliposikia mazungumzo yetu waliweza kudhani na mimi ni mfanyakazi wa pale, wakaanza kuniomba niwasaidie changamoto zao.

Zile fomu zao nimejaza mara 7 kwa vipindi tofauti tofauti, na kila unapoenda kuulizia mrejesho ofisini kwao wanakupa ujaze tena zile fomu kwa ahadi ya kuwa atakuja surveyor.

Ukijaza tu zile fomu na we ukatoka basi shughuli inaishia hapo yani ni kama walikuwa wanakusubiria uondoke ili waendelee na mambo yao.

Baada ya miaka miwili kupita nikaona kwenye website yao wameweka mfumo wa ku request huduma ya fiber kwa njia ya mtandao.

Nikajiwazia huwenda hii ya kwenye mtandao ndio njia sahihi, huko nako nikatuma maombi, baada ya wiki mbili nikacheki status nikakuta verified.
 
Kilichoendelea baada ya hapo ikawa ni kimya.

Nikatuma maombi mapya napo majibu yakawa hivyo hivyo na ukifuatia ukimya wa muda mrefu.

Nikawacheki kwenye WhatsApp number yao, wakaniomba niwaoneshe fomu ya online niliyojaza, nikawatumia wakasema wamemfikishia surveyor nisubirie atanicheki kuja location.

Mwezi ukapita kimya bila huyo surveyor kupiga simu, nilipowarudia tena WhatsApp wakaniona kero hata meseji yangu hawakuijibu.

Nilipoona hapo bado kuna ugumu nikawaza pengine huu ugumu unatokana na hawa watu wa chini, nikawaza huwenda ngazi za juu hawana taarifa na hiki kinachofanyika kwenye ofisi zao.

Nikatuma emails za malalamiko ambazo zilienda Head Quater, Head Quater wakanijibu kwa meseji ya samahani na kisha wakani direct kwenye ofisi ambazo zipo ukanda wangu wakamkabidhi mmoja wa wafanyakazi ashughulikie swala langu mpaka mwisho, na wakaniomba niwe nawapa mrejesho.
 
Hapo kidogo nikaona nuru.

Kweli kesho yake walikuja kufanya survey lakini team iliyokuja niliweza kubaini kuwa haikuwa na watu wenye expertsm ya maswala ya fiber.

Wakawa wananiuliza "kwani hapa fiber imeishia wapi" nikashangaa yani wao wanaohusika na fiber hawana taarifa ya miundombinu yao?

Wakaniambia kuwa fiber itakuwa ipo mbali kidogo na sehemu ambayo nipo hivyo watachora ramani ya makadirio kujua ni nguzo ngapi zinahitajika ili kuweza kufunga hizo nyaya za fiber kunifikia nilipo.

Hapo tena nikawauliza"kwenye kampeni yenu ya fiber mlangoni mbona serikali iliingia ubia na TANESCO kushea nguzo ili kurahisisha usambazaji wa fiber?"

Wakajibu kuwa sio kila muda tuna share nguzo na TANESCO kuna muda tunakuwa limited.
 
Baada ya hapo nikaja kuambiwa kuwa eneo langu kifaa cha kuunganishia fiber kimejaa hivyo engineer wao yupo kwenye process ya kutengeneza kingine.

Hiyo ilikuwa ni Septemba mwaka jana.

Mpaka leo hicho kifaa bado engineer anakitengeneza.

Nikaona bora nichukue Router ya Airtel ambayo mpaka sasa naweza kusema ndio option bora kwasababu inakupa extra benefit ya kuweza kuitumia popote lakini advantage nyingine ni kuwa na uhakika wa kupata huduma hata pale umeme unapokuwa umekatika kwasababu ina battery yenye reserve ya ku store charge kwa masaa zaidi ya 8.
 
Ndugu zao na DAWASA, wavivu sana wa kufikiri. Ni karibia mwaka sasa huduma ya maji hatujapata tangu tufanye maombi ya kuunganishiwa. Hovyo kabisa.
 
Pole sana Mkuu ila hiyo TTCL ni janga la wengi sana. Kwanza hawakupi jibu la usahihi, majibu yao ni kuzungusha. TTCL ilikuwa na nafasi nzuri sana ya kufanya vizuri kwenye hii huduma ila ndio hivyo hawatumii akili kabisa
 
Ajira ningi kwa wafunga faiba ni mkataba wa mwaka mmoja tu, mkataba ukiisha wanaweka vijana wengine sotegemea kukuta imu nzima nzima tangu wanazaliwa mpaka wanakua hawaijui hiyo faiba inafungwaje sababu woe pale ili mradi mkono uende kinywani
 
Ajira ningi kwa wafunga faiba ni mkataba wa mwaka mmoja tu, mkataba ukiisha wanaweka vijana wengine sotegemea kukuta imu nzima nzima tangu wanazaliwa mpaka wanakua hawaijui hiyo faiba inafungwaje sababu woe pale ili mradi mkono uende kinywani
TTCL ni miyeyusho

Unaomba huduma ya fiber lakini unavyozungushwa ni kama umeomba kupewa hisa za kampuni bila kulipia gharama yeyote
 
Halafu kuna mtu anatuletea roboti hajui kinacho endelea huko?
 
Inategemea na ulipo, isije ikawa upo km 5 toka ilipopita ikawa ni gharama sana kukufikia. Sisi tuliopo dodoma tunaenjoy tu
 

Hawakupi labda uwe na kadi ya chama
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…