Trump aiambia Russia ichague mazungumzo na Ukraine au vikwazo zaidi hadi ifilisike kabisa

Imeloa

JF-Expert Member
Jan 28, 2013
14,698
17,841
Rais wa Marekani, Donald Trump, amemwonya Rais wa Urusi, Vladimir Putin, kumaliza "vita vya kipuuzi" nchini Ukraine au akabiliwe na ushuru mkubwa na vikwazo zaidi.

Kupitia jukwaa lake la Truth Social Jumatano, Trump alisema ana uhusiano mzuri na Putin lakini akasisitiza kuwa ni wakati wa kumaliza vita hivyo. Alisema vita hivyo visingetokea kama angekuwa Rais na kuongeza kuwa hakuna maisha zaidi yanayopaswa kupotea.

Trump alionya kuwa ikiwa makubaliano ya kusitisha mapigano hayatafikiwa haraka, atalazimika kuweka ushuru na vikwazo vikali kwa bidhaa zote kutoka Urusi kwenda Marekani na nchi nyingine zinazoshirikiana.

Aidha, alikumbusha mchango wa Urusi katika kushinda Vita vya Pili vya Dunia lakini akasisitiza kuwa Urusi lazima imalize vita hivyo sasa, vinginevyo hali itakuwa mbaya zaidi.

Serikali ya Biden tayari imeweka vikwazo vingi dhidi ya sekta mbalimbali za kiuchumi za Urusi, ikiwemo mafuta na nishati, ili kuzuia fedha za kufadhili vita hivyo.


=============================================================

US President Donald Trump has warned his Russian counterpart Vladimir Putin to end the 'ridiculous war' in Ukraine or face high tariffs and further sanctions.

Trump, who was sworn in as the 47th President of the United States on January 20, said this on Truth Social on Wednesday, a social media platform owned by him.

Trump called out Russian President Putin by name in the social media post, arguing that he always had a good relationship with the leader, but that it was time to settle "this ridiculous War!"

Asserting that he is looking to hurt Russia, Trump said he wants no more lives to be lost in the war.

“Let's get this war, which never would have started if I were President, over with! We can do it the easy way, or the hard way - and the easy way is always better. It's time to “MAKE A DEAL.” NO MORE LIVES SHOULD BE LOST!!!” Trump said.

“I love the Russian people, and always had a very good relationship with President Putin - and this despite the Radical Left's Russia, Russia, Russia HOAX. We must never forget that Russia helped us win the Second World War, losing almost 60,000,000 lives in the process,” he said.

He also warned that if there was not a ceasefire deal soon, he would “have no other choice” but to impose tariffs, taxes and sanctions on “anything being sold by Russia to the United States, and various other participating countries.”

“All of that being said, I'm going to do Russia, whose Economy is failing, and President Putin, a very big FAVOUR. Settle now, and STOP this ridiculous War! IT'S ONLY GOING TO GET WORSE. If we don't make a “deal,” and soon, I have no other choice but to put high levels of Taxes, Tariffs, and Sanctions on anything being sold by Russia to the United States, and various other participating countries,” Trump said making an open appeal to the Russian leader.

The Biden administration has already imposed numerous sanctions on various Russian economic sectors, including its oil and energy sectors earlier this month, in an effort to cut off its revenues to fund the war in Ukraine.

Source: Daily Pioneer
 

Attachments

  • Trump.png
    Trump.png
    281.2 KB · Views: 1
  • Trumpp.png
    Trumpp.png
    218.2 KB · Views: 1
Usa amflisi mrusi kwa vikwazo?!!
Ndio, na sio directly, na haswa kama unaelewa mfumo wa oil pale russia.
Trump anaweza piga hesabu zake vzuri russia akashindwa kuuza mafuta yake. Mfsno sahvi , china kashaanza kukimbia mafuta ya russia. Marekani ikiamua ndani ya kipindi kifupi, mrusi atashindwa kuuza mafuta yako, hivo kufanya akose storage na kuuza mafuta kwa bei ya chini sana na end of the day, uchumi wake ukadondoka maana anategemea sana mafuta kupata revenues. Iko ni kimoja kidogo sana ila kikubwa kwa russia.
 
Una dhani ni vikwazo gani ambavyo zina weza kuiathiri urusi kwa sasa?
Hivyo hivyo vichache vilivyo baki anakazia pia kingine anaweza ongeza kuwapa Ukraine silaha zaidi za kisasa kwa ajili ya kuwatia hasara Urusi kama ambavyo kwasasa unasikia wanapiga tu ndani mule Urusi, maana kenge hawezi kuona kaumia mpaka aone damu
 
Hivyo hivyo vichache vilivyo baki anakazia pia kingine anaweza ongeza kuwapa Ukraine silaha zaidi za kisasa kwa ajili ya kuwatia hasara Urusi kama ambavyo kwasasa unasikia wanapiga tu ndani mule Urusi, maana kenge hawezi kuona kaumia mpaka aone damu
Acheni ujinga, Trump ni mjinga kama wajinga wengine. Dunia sasahivi imebadilika sana. Vikwazo vimedunda ktk nchi ndogo kama North Korea na Iran ndio vije viweze kwenye taifa kubwa kama Russia?
 
Acheni ujinga, Trump ni mjinga kama wajinga wengine. Dunia sasahivi imebadilika sana. Vikwazo vimedunda ktk nchi ndogo kama North Korea na Iran ndio vije viweze kwenye taifa kubwa kama Russia?
Urusi ameathirika sana wewe unafikiri pesa yote ile anayo peleka jeshini ingekuwa inakwenda kwenye maendeleo wange sogea kwa kiasi gani? watu wanajua uchumi wa Urusi uko vibaya sio ule wa kabla ya vita , sasa ameshapewa OFA ni yeye Putin kusuka au kunyoa , iran uchumi wake sio mzuri ndio maana hakuwa na msaada kwa Assad kipindi hiki, huyo North Korea ndio hamna kitu anapeleka wanajeshi wake kufa Urusi ili apate msaada

E25EB268-D6C6-4ED0-BF9F-08596781F0E1.png
 
Back
Top Bottom