Transfer za loan

avi.JNR

Senior Member
Nov 17, 2015
139
87
Hivi wanachuo waliofanya transfer bado yanaendelea kula unga na maji wanalala Vyuoni wakiwa na maisha magumu sana.

JE nani wa kuwashika mkono...Ikiwa wamevumilia wamefata taratibu kwa kusubiri siku 60 na mpaka sasa zimeisha, sasa tunataka pesa kwa NJIA YOYOTE Tumechoka.

Kama kuingia barabarani poa tu bwana hatuna JINSI.
 
Fedha za wale wa transfer huja pamoja na za waliofanikiwa ktk appeals, na ni mwanzoni mwa semester 2.
 
Kiukweli swala la transfer limekuwa ni tatizo kubwa namuomba muheshimiwa waziri wa elimu Prof Ndalichako ili kulitatua hili atumie njia zifuatazo 1.Awaagize ma loan officer wote vyuoni wampelekee majina ya wanafunzi waliofanya transfer yakiwa na Jina la mwanafunzi kozi anayosoma Reg No pamoja form inayoonesha mkopo wa kila mwanafunzi ulipoenda. x2.Akishapata vielelezo hivyo vya kila mwanafunzi prof ndalichako awaagize bodi kupitia vielelezo hivyo ndani ya siku 2 wawe wametatua tatizo hili lisilo na wanafunzi wanaozidi 500. x3.Kwa nini nasema hivyo bodi ya mikopo wamekuwa ni wazembe wametupa siku sitini wawe wametatua tatizo letu lakini mpaka Leo kimya .Prof ndalichako hali ni mbaya sana tunalala njaaa huku mikopo yetu ikiwa ipo.Naomba utusaidie na mungu atakubariki.
 
Mm nadhani maneno yako yana maana sana ndani yake ..haswa kwa watu tukio katika janga huku..sasa kama siku sitini zimeisha kwann tusiende kuhoji pale kwao jamani?? Sisi ni watu wenye akili sasa .tufanye maamuzii ..kwani mkuu upo CHUO GANI? na ni wangapi wamefnya transfer hap0?? Wahimize hapo inawezekana tumesahaulika ..tushavumilia vya kutoshaa
 
Fedha za wale wa transfer huja pamoja na za waliofanikiwa ktk appeals, na ni mwanzoni mwa semester 2.
Noted but...hatuwez kusubiri kwakuwa tuna history tofauti kwakuwa wao WANAPATA hela na sisi hatujapata hata kumii
 
Heshima yako Prof .Ndalichako.Kwa niaba ya wanafunzi wa vyuo waliofanya transfer ya mikopo yao ya elimu ya juu hii ikiwainajumuisha wale mikopo yao ilienda vyuo vingine tofauti na vyuo walivyo chaguliwa na wale waliohamia vyuo vingine bodi huwajumuisha kama transfer.
Transfer profesa Ndalichako limekuwa ni tatizo kubwa kwa bodi ya mikopo walituahidi siku sitini watakuwa wametatua tatizo hili lakini mpaka sasa hawajatatua wiki mbili zilizopita ilikuja taarifa kutoka bodi kuwa tuandike Reg No,pamoja na Account No za Bank lakini mpaka sasa profesa Ndalichako hamna kinachoendelea.
Napenda kukukumbusha Prof Ndalichako kuwa naibu wako mwezi uliopita alikaaa na uongozi wa jumuiya ya vyuo vikuu kikao kilichofanyikia chuo kikuu cha Dar es salaam na moja ya mambo waliyo zungumzia ni pamoja ya transfer ya mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu ambapo katika majibu yake alijibu kuwa ndani ya wiki mbili tatizo litakuwa limetatuliwa lakini mpaka sasa kimya .
Madhara ya kuchelewesha mikopo ya wanafunzi ambayo kwa uzembe wao bodi ya mikopo waliipeleka sehem nyingine pamoja na wale waliohama toka chuo kimoja kwenda kwingine ni kama ifuatavyo
1.Wanafunzi kuathirika kisaikolojia kwa kuahidiwa ahadi zisizo kuwa na majibu.
2.Madonda ya tumbo kwa kulala na njaa kwa sababu wazazi wameshatangaziwa kwenye vyombo vya habari kila mwanafunzi alishapata mkopo wake kumbe wanazungushwa kila siku.
3.Kushindwa kufikia malengo yao.
4.Kujiingiza kwenye biashara ya ngono kwa wasichana.Kutokana na kuchelewa kuwaletea mikopo yao.
Hayo ni machache tu Profesa Ndalichako suluhisho la tatizo hili muheshimiwa waziri ni kama ifuatavyo:-
1.Kutoa agizo kwa maafisa mikopo wa vyuo(loan officer) kuwa waandike majina ya wanavyuo wote mikopo yao ilioenda sehem nyingine ,Reg No,pamoja na Maelezo yanayoonesha sehem mikopo ilipoenda kwa kila mwanafunzi na Kisha waiwasilishe kwako profesa.
2.Baada ya hapo Profesa ndalichako nakuomba kwa kutumia nondo hizo waagize bodi ya mikopo walishughulikie tatizo hilo ndani ya siku mbili kwani ni tatizo la wanafunzi wasiozidi 500 nchi nzima.
3.Wakishindwa kutatua tatizo hilo kwa muda uliowapa muheshimiwa Ndalichako nakuomba unshauri Raisi awafukuze kazi kwani sisi mazara tunayoyapata kusubiri ni makubwa sana.

NB.Profesa ndalichako nakuamini naomba utusaidie kutatua tatizo hili Mimi nanyanyasika sana mkopo wangu kuchelewa nalala njaaa na pia nashindwa kuhuzuria mpaka vipindi.Mungu akubariki Prof Ndalichako.

Eeeeeee mungu Tusaidie ..................
 
Waziri wa elimu au mamlaka husika tunaomba mtusaidie tumechoka kulala njaaa hapa nilipo sijala yaaani tunateseka sana na wazazi walishajua tulishapata mikopo.
 
Waziri wa elimu anatumbu jipu kubwa la gpa. Hilo lenu la kulala na njaa ni dogo na halina umuhimu.
 
Mkuu be serious watu tunalala njaaa na mikopo yetu ipo vyuo vingine kuihamisha unasema haina umuhimu tukuelewe VP?Wewe ni pathetic.
 
Sio kama mimi siko 'siriasi', ila waziri wenu ndiye ambaye hayuko siriasi.
Wanafunzi mnateseka, yeye yuko 'bize' na gpa. Hawa mawaziri wetu wa elimu, utadhani kazi zao ni kusimamia necta tu. TCU, NACTE, TIE, HESLB NACTE n.k, vyote viko chini yake, ila yeye yupo bize na pga tu, bila kuwajali mnaopata madonda tupo kwa sababu ya njaa.
 
Reactions: j m
Inauma sana! Semester inaisha boom naskia kwa redio tyuuuu... Nadaiwa kuliko serkal ya Tz.. Cjui serikali ipoje.
Transfer zikko tayari ila makato mengi kama vile tunakatwa kodi na bado mm sjapata jina langu kati ya Yale yaliyotoka board
 
Jaman, sis pesa hadi lin!? Kwanin ma loan officer wa Saut wanazingua Sana, unakuta anajifungia ofcn Sasa sijui tufanye nini!?
 
Jaman, sis pesa hadi lin!? Kwanin ma loan officer wa Saut wanazingua Sana, unakuta anajifungia ofcn Sasa sijui tufanye nini!?
Ndugu yangu #mpambalachuma #maisha ni kupambana brother tatizo sio ma loan officer jipu lipo idara ya allocation Bodi ya mikopo pamoja na malipo ndo wasumbufu wanatulaza njaaa inaniuma sana ila mungu awabariki.
 
Jaman, sis pesa hadi lin!? Kwanin ma loan officer wa Saut wanazingua Sana, unakuta anajifungia ofcn Sasa sijui tufanye nini!?
Kuna kitu hamkijui ila ukienda loan board utajua mengi .na mkiwasubiro ma loan officers mnaweza pata Ella 2017 ..nmeenda BOARD nimejua mengi asee
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…