Jamani hizi dini zinaconfirm kabisa kuwa ziko kibiashara na hao wachungaji wako kibiashara zaidi. Mi nilidhani kipaumbele kwa mchungaji kama mtumishi wa mungu ni kanisa.
Pale kwa Gwajima hamna kanisa yaani ni kama hana mpango kabisa maana anajua kikisanuka atabaki na asset zake kama train na helicopter.
Angalieni makanisa yanayohubiri katika roho au yaabuduyo Mungu kama Catholic na KKKT vipaumbele ni kuinua makanisa waumini wasali pazuri siyo unasali kwa wasiwasi jengo linaweza kukubomokea.
Pale kwa Gwajima unasali ukiwa unachungulia pakutokea maana linaweza dodoka muda wowote.
Jamani angalieni dini za kweli achaneni na dini za biashara.
Ni hayo tu
Umetumia kiasi tu cha akili yako kufikiri, lakini hukujiuliza maswali ya kutosha ilikujua kwanini hiyo reli na treni?, Maisha ni kupanga na kupanga ni vipao mbele, kama treni itaboresha zaidi maisha ya kanisa kuliko jengo basi hicho ndicho cha kuanza nacho.
lakini pia kumbuka kumwabudu Mungu sio kwenye jengo zuri, lakini nikatika uwepo wake. Jengo zuri halikuhikishii uwepo wa Mungu japo ni jambo zuri kuwa na jengo zuri lenye uwepo wa MUNGU, na watu wengi wameenda kwenye majengo mazuri lakini hawakuenda kwenye madhabahu zenye moto wa MUNGU. Vitabu vitakatifu vinatuonyesha MUNGU aliwatokea watu katika sehemu hata siziso pendeza, lakini ndivyo alivyochagua yeye, na cha ajabu watumishi waliofanya sana kazi ya MUNGU kwenye vitabu ni wale ambao maisha yao yalikuwa ya mapangoni, nyikani na sehemu sizizopendeza kama akina Yohana, Samsoni, Paulo nk.
Tunacho cha kijifunza hapo, kila ulipo hakikisha roho yako inakushuhudiwa kuwa hapo ulipo pana nguvu ya Mungu na sio mashairi ya waandishi na ujuzi wa Mwanadamu katika kusema maneno ya MUNGU.
Ili kukidhi idadi ya waaumini wanaokuja ufufuo na uzima upo mpango wa kujenga kanisa nje ya mji, ambako huko eneo lakutosha kanisa la mita 300 kwa 100 na huduma nyingine limepatikana, hivyo kurahisisha usafiri wa waamini, ndipo wazo la kuwa nausafiri wa treni linakuja. Hata kama litatoa huduma kwa jamii lakini pia lengo kuu ni hilo.
Na katika swala la maendeleo, wazo huja kwanza, ndipo resources zinaanza kutafutwa, hivyo wakati mwingine mawazo yasizue watu kufikiri na kujaribu kusonga mbele, wengi tunataka tupate hela kwaanza ndo tuwaze cha kufanya, nadhani ndiyo maana tunakuwa masikini sana, kwa sababu muda ukiwa na hela bila wazo ni rahisi kuharibu hiyo pesa au kuipeleka kusiko. Hata kama hunapesa usiache kuwaza mbali na kuja na fikra zitazokusukuma kupata pesa na mambo kutokea. nadhani ndiyo falsafa ufufuo na uzima wnaijenga na ndivyo pia MUNGu anatamani tufanye na ndiyo haswaa maana ya imani katika kristo.