Trafik Geita wembe ni ule ule, Kamanda Mpinga tumbua majipu

Muna117

Member
Dec 31, 2012
20
1
Mbali na jitihada mbali mbali zinazofanywa na serikali kuondoa rushwa na kuongeza mapato serikalini, lakini bado trafic wetu nao wanabuni mbinu mbali mbali kuhujumu mapato ya serikali na kujiongezea kipato isivyo halali.
Serikali imehakikisha inanunua kamera kuzibiti mwendo (Tochi) kwa ajili ya Trafic kuwadhibiti wanaokwenda mwendo kasi sehemu ambazo spidi ya magari inatakiwa iwe ndogo kulingana na sehemu husika, lakini cha kushangaza yanatokea haya ambayo nimeyashuhudia leo.
Nikiwa natokea Bukoba asubuhi maeneo ya mkoa wa Geita mbele ya Kasamwa nilisimamishwa na trafic akiyekuwa na kamera na kunitaka nilipe fine kwa kuzidisha mwendo, kamera yake (Tochi) ilionyesha ninilikuwa na speed ya 83 kwa saa badala ya 60 zinazotakiwa. Wakati nipo katika harakati za kulipa fine ilikuja basi namba 1 (jina kapuni) kutoka Mwanza ikielekea Bukoba ikiwa kasi, lakini cha kushangaza yule Trafic mwenye kamera hakuimulika hiyo basi kutaka kuhakikisha mwendo wa basi hilo, Basi lilipomkaribia alilisimamisha na kwenda kwa dereva dirishani na kupena mkono na huyo dereva na kisha kupeana kitu ambacho trafic alikiweka mfukoni na kuagana na huyo dereva kwa tabasamu kali huku trafik akimwambia usinitibulie huko mbele (akimaanisha asiwape ishara wanaokuja kuwa wapo hapo). Baadae tena muda mfupi kidogo likaja basi lingine namba 2 (jina kapuni) nalo lilikuwa kasi, hakulimulika pia, Akalisimamisha akatoka nadhani ni konda yule wakasima mbele ya basi ambapo si rahisi abilia kuwaona na trafik kupewa pesa, nilishuhudia akirudisha na chenji, Duh! Nilishangaa sana nikamuuliza yule trafik aliyekuwa akiniandikia fine mbona hayo mabasi hayakumulikwa Tochi? Akajibu spidi yake yote mawili ilikuwa ndogo inaonekana kwa macho, kitu ambacho sio kweli, akanionyesha unaona kuna basi limepita super sumi wamelipa, nikamjibu inaelekea nyinyi mnamabasi yenu ambayo mnapeana chochote na hivyo hamyamuliki kujua spidi yake, hakujibu.
Kamanda Mpinga kazi kwako, majipu hayo.
 
Hiyo ni cha mtoto maana naamini kama zitapigwa kura za maoni juu ya taasisi gani ya umma inayoongoza kwa rushwa, basi taasisi ya jeshi la polisi linaweza kuibuka kidedea. Jambo la msingi ni kwa serikali kuboresha mazingira ya kazi hususani mishahara na stahiki nyinginezo. Vile vile kuna haja kubwa ya kuwafanyia uhamisho maofisa waliokaa muda mrefu katika vituo vyao vya kazi.
 
Rushwa ni donda kwa taifa, kupona kwake lazima kovu libaki, kwahvyo kuisha kwa rushwa never.
 
Sasa na wewe ulilipa faini kuongeza pato la serikali au ulijizugisha kisha ukatunisha mfuko wa afande?
 
Sasa na wewe ulilipa faini kuongeza pato la serikali au ulijizugisha kisha ukatunisha mfuko wa afande?
Nililipa kuichangia serikali maana alinipa na notification, ingawa nilipo muomba risiti alisema mpaka turudi geita kwa muhasibu au nimpe namba yangu ataituma central police Mwanza.
Unajua hizi tochi za sasa kama ikisha kumulika tu hawana uwezo wa kuifuta mpaka katika server yao, ndio maana yale mabasi mawili hawakuyamulika ili yasiwemo katika tochi yao.
 
Jamaa wanakuwaga na vitabu vyao hao. Na siku hizi anakukomalia hasa utafikri kweli inaingia kwenye mapato ya serikali kumbe icho kitabu ni copy of the original.
 
Hiyo ni cha mtoto maana naamini kama zitapigwa kura za maoni juu ya taasisi gani ya umma inayoongoza kwa rushwa, basi taasisi ya jeshi la polisi linaweza kuibuka kidedea. Jambo la msingi ni kwa serikali kuboresha mazingira ya kazi hususani mishahara na stahiki nyinginezo. Vile vile kuna haja kubwa ya kuwafanyia uhamisho maofisa waliokaa muda mrefu katika vituo vyao vya kazi.
Tafiti Za miaka yote bandari haikuwahi kuwa hata top 20 lakini baada ya majipu kutumbuliwa ndio tuna jua kuwa kumbe wenyewe ndio namba moja kumbe polisi Sawa na wezi wa simu na kuku alafu hao wengine ndio majambazi
 
Back
Top Bottom