Nifah
JF-Expert Member
- Feb 12, 2014
- 34,095
- 79,625
Jioni ya leo February 26 kutakuwa na kilele cha msimu wa pili wa tuzo za muziki zinazojulikana kama Trace Awards huko visiwani Zanzibar.
Tukio hilo litakalofanyika viunga vya hadhi ya juu kistarehe, Mora Resort zitahudhuriwa na mastaa wakubwa Afrika wakiwemo Davido, Rema, Fally Ipupa, WizKid, Diamond Platnumz, Burna Boy, Ali Kiba, Zuchu na wengineo.
Msanii wa hapa nyumbani kwetu Diamond ameonekana kuziteka tuzo hizo kwa kupendekezwa katika vipengele vingi zaidi, huku Zuchu, Ali Kiba, Abigail, Mboso pamoja na mwanamuziki wa Injili Bela Kombo wakiambulia vipengele vichache.
Nitakuwepo hapa kuwapa updates zote, kuanzia drama za kwenye red carpet hadi kwenye unyakuaji wa tuzo.
We here, LIVE.
Muhimu
Tukio hili litaruka LIVE kupitia DStv Channel 323, Wale wa Azam walisema watarusha live pia Channel 174 pamoja na 106.
View: https://www.youtube.com/live/iAf5Zl1_yos?si=aEZiOmBpHlbvWMl-