Mwana Mpotevu
Platinum Member
- Sep 7, 2011
- 3,295
- 2,500
Mamlaka ya mapato Tanzania inadaiwa kuifungia Radio Free Africa ya Mwanza inayomilikiwa na Antony Dialo kutokana na kudaiwa kodi kubwa.
Ofisi za Kampuni ya Sahara Media Group inayomiliki vituo vya Star Tv, Radio Free Africa (RFA) na Kiss FM zimefungwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kufuatia kudaiwa malimbikizo ya Tsh 4.5 bilioni.
Ofisi hizo zimefungwa leo Alhamisi (Julai 13) na wakala wa TRA, kupitia Kampuni ya udalali ya Sukah Auction Mart and Court Brokers ya jijini Mwanza.
Meneja Utumishi na Utawala wa Sahara Media Group, Raphael Shilatu amethibitisha kuwa ni kweli ofisi hizo zimefungwa sababu wan malimbikizo ya madeni yanayotokana na kuhama kutoka mfumo wa analojia kwenda dijitali.
Lazima tukiri kwamba mmeshuhudia TRA wamefunga maeneo yetu ya kazi na hii inatokana na malimbikizo ya kodi ambayo siyo ya sasa ni ya muda mrefu hata nyie waandishi wa habari mnajua kwamba kadri uwekezaji unavyokuwa mkubwa ndivyo gharama zinazidi kwenye uwekezaji. So, ilitulazimu kutafuta fedha kwenye mabenki ili tuweze kukidhi matakwa ya Serikali ya kuhama analogy kwenda Digatal.
“Niwatoe wasiwasi Watanzania na wapenzi wa Sahara hili ni jambo la muda lakini kampuni yetu inafanya jitihada kuhakikisha kwamba haya yanamalizika vyombo vyetu virudi hewani.” amesema Rafaeli Shilatu
TRA wamewaondoa studio wafanyakazi wote na kuifunga radio hiyo. Kwa sasa ukiwasha radio utasikia matangazo ya kiingereza ya BBC.
Diallo ni mwenyekiti wa CCM Mwanza na anadaiwa mamilioni ya kodi na TRA miaka mingi.
Star Tv pia imekumbwa na sekeseke hilo. Ikumbukwe hii ndio TV pekee binafsi iliyokuwa ikipingana na MOAT na TEF katika sakata la RC Paul Makonda na walirusha kipindi maalum cha Makonda huku Jumuiya ya Wanahabari wakitangaza rasmi kujitenga na maswahibu yoyote yatakayokuja kuikuta RFA na Star TV.