TRA kuyapiga mnada magari zaidi ya 400

Salary Slip

Platinum Member
Apr 3, 2012
49,326
152,138
Hii ni habari katika ukurasa wa mbele wa gazeti la Uhuru la siku ya leo.

Binafsi sijasoma hilo gazeti bali nimeona hiyo heading hivyo sijui kama magari hayo yako bandarini na wahusika wameshindwa kuyakomboa au ni ni magari ya biashara mimi sielewi.

Swali:All in all,hali hii tafsiri yake ni nini?

======

Magari zaidi ya 400 jijini Dar es Salaam ambayo wamiliki wake wameshindwa kuyalipa, yako hatarini kupigwa mnada na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).

Magari hayo, hayajalipiwa kodi na tozo mbalimbali ikiwemo leseni ya matumizi ya barabara (Road Licence)

Pamoja na magari hayo pia shehena ya mali mbalimbali zinazoshikiliwa kutokana na wamiliki wake kukwepa kodi, nazo huenda zikadaiwa.

Katika mali hizo, zimo nyumba tatu za nfanyabiashara maarufu, Said Lugumi baada ya kushindwa kulipa kodi ya TZS. bilioni 14 katika kipindi cha wili mbili alichopewa na TRA kuelekea ukingoni.

Kwa mujibu wa taarifa za uhakika zilizotufikia, magari ambayo yatapigwa mnada ni yale ambayo yalikamatwa na TRA kupitia wakala wake wa ukusanyaji kodi kampuni ya usalali ya Yono Auction Mart.

Magari hayo ni mabasi, malori na mengine madogo ambayo wamiliki wake ni kampuni za watu binafsi.

Habari hizo zinaeleza kuwa, magari hayo yamehifadhiwa katika maeneo mbalimbali jijini Dar es Salaam, likiwemo eneo la kuhifadhia magari lilomilikiwa na Wakala wa Ufundi Umeme (TAMESA), lililopo Gerezani na Bahari Beach.

Kati ya nyumba tatu za Lugumi mbili ziko Dene Beach na moja mtaa wa Mazengo, Upanga, jijini Dar es Salaam.

Inadaiwa asilimia kubwa ya wamiliki wa magari hayo ni wale waliokuwa waliyamiliki kwa kutumia fedha za dili hivyo wameshindwa kuyagomboa baada ya serikali kuziba mianya ya matumizi ya fedha.

Baadhi ya wamiliki wameshuhudiwa wakihaha katika maeneo yalipohifadhiwa magari hayo, baada ya kusikia yako kwenye hati hati ya kuuzwa kwa bei chee na TRA kupitia Yono.

Akizungumza na waandishi wa habari, jijini Dar es Salaam jana, Mkurugenzi Mtendaji wa Yono, Scholastica Kevela, alisema kampuni yake inasubiri maelekezo ya TRA ili kukamilisha zoezi la kuuza mali hizo.

“Mali ambazo tunatarajia kuziuza ni magari zaidi ya 300 hadi 400 ambayo hayajagombolewa kwa muda mrefu na wamiliki. Magari hayo, yalikamatwa kutokana na wamiliki wake kukwepa kodi ya tozo ya leseni ya barabara,”alisema Scolastica.

Alisema mwezi uliopita pekee TRA kupitia Yono ilifanikiwa kukamata magari 15,000 kutokana na makosa mbalimbali, baadhi ya wamiliki waliyagomboa.

“Haya yaliyobaki tunasubiri maelekezo ya TRA ili tuweze kuyauza kwa mnada kwa sababu taratibu zinaeleza bayana kwamba mdaiwa akishindwa kulipa baada ya siku 14, mali yake iliyokamatwa itauzwa kwa mnada.” alisema mkurugenzi huyo.

Alisema Rais Dk. John Magufuli anasisitiza kodi ndiyo mhimili wa kuendesha nchi. Hivyo, wakwepa kodi hawa tunawahesabia kama wahalifu wengine. Wale wenye uwezo wa kuja kuyakomboa, wafanye hivyo haraka, kwa sababu, mahali ambapo mkwepa kodi yupo na sisi tupo,”

Alisema maeneo ya kuhifadhia magari yaliyokamatwa na TRA kupitia Yono yako mengi, huku kampuni hiyo ikiingia gharama ya kulipa ushuru wa hifadhi.

“Hatuwezi kuendelea kuingia hasara na pia serikali inahitaji kodi ilipwe ili fedha za maendeleo zipatikane. Muda tuliowapa wengi umekwisha,” alionya mkurugenzi huyo.

Mbali na magari hayo, alisema kupitia TRA, Yono inashikilia shehena kubwa ya mali za wafanyabiashara ambao wanakwepa kutumia mashine za EFD.

“Mali nyingi ni za thamani kubwa. Hizi zimehifadhiwa. Tutauza kwa maelekezo ya TRA” alisema.

Kuhusu hatima ya mali za Lugumi, mkurugenzi Kevela alisema wanasubiri maelekezo ya TRA kabla ya hatua nyingine.

“Mbali na Lugumi, mfanyabiashara mwingine ni G. Dewji ambaye anadaiwa na serikali TZS bilioni 1.8 na kampuni ya Mutluhan Construction Industries inayodaiwa TZS. bilioni 45,” alifafanua.

Credit: Swahilitimes
 
Reactions: 7ve
Kitu chochote kikiuzwa na TRA, maana yake unadaiwa kodi ya ushuru wa forodha.

Hii maana yake watu waliagiza magari, lakini wakashindwa kuyalipia ushuru.

Angalia list kwenye link hapo chini, utashuhudia mengi ya magari hayo ni ya makampuni ya magari ambayo zamani walizoea kukwepa kodi!. Magari yalikuwa yakitolewa na kuhifadhiwa kwenye ICDs or Bonded Customs Warehouses , kisha watu hucheza dili na TRA kukwepa ushuru. Lakini sasa wameamua hakuna mizigo kwenda ICDS hadi Bandarini pajae, hivyo hizo gari zimeshindwa kuondolewa kimchoro mchoro.

Ila pia kuna magari ya watu ambao wameagiza na walidhamiria kuyalipia ushuru genuinely lakini kufuatia mdororo wa uchumi, na hii hali ya ukata wa magufulision, hivyo magari yamewasili, watu wakajikuta hawana pesa za kuyakomboa.

Tangazo rasmi ni hili na list iko kwenye link.

Paskali


CUSTOMS AND EXCISE DEPARTMENT

This is to notify the general public that the under listed goods will be sold by public auction or disposed of in a manner the Commissioner for Customs and Excise may deem fit if they remain un-cleared from the Customs area within thirty (30) days from the date of this notice.

The Auction Sales will be conducted at MISUGUSUGU, LW9, AFRICAN ICD, JEFAG, ECLS ICD, SHINYANGA and ZANZIBAR from 10:00 am on the dates and places as shown below:-

  1. Monday the 05th June, 2017 – LW9, MISUGUSUGU, SHINYANGA, ZANZIBAR, DIAMOND MOTORS, NOBLE MOTORS, AFRICARRIERS and CHICASA.
  2. Thursday the 08th June, 2017 – ECLS ICD, CARVIEW JAPAN, AUTO-SUECO, QUALITY MOTORS, ALLIANCE AUTOS, TANZANIA 4 BY 4, HARAB MOTORS and TAHIR TRADING.
  3. Monday the 12nd June, 2017 THE LAND LTD, MANTRACK, DAR MART, CHATHA MOTORS, NDEGE ADVOCATES AND JEFAG and MUTESIGWA KATULANDA.
The goods may be viewed by the public during working hours two days before the day of the auction. For more details please visit our website www.tra.go.tz.


CONDITIONS OF SALE

  1. Successful bidders will be required to pay 25% of the purchase price on the spot. The remaining 75% must be paid within 48 hours after the auction sale;
  2. Any person who makes the highest bid and fails to pay the mandatory 25% of the purchase price on the spot will be charged for the interference with the auction process with malicious intension and stern legal measures will be taken against such person;
  3. Goods will be sold in lots of full consignments; and
  4. Goods shall be withdrawn from the auction upon full payment of the respective duties and taxes.




Qamdiyay Akonaay

Ag. COMMISSIONER FOR CUSTOMS AND EXCISE



List of overstayed goods to be auctioned
 
Mkuu,asante kwa taarifa hii.
 
Hii nchi ya viwanda itaua watu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…