TRA Kilimanjaro kitengo cha leseni fanyieni kazi kero za watu

kisinja

JF-Expert Member
Sep 30, 2013
241
295
Kwa kweli TRA Kitengo cha Leseni Kilimanjaro mnahitaji kujitathmini. Leo niliambiwa kuja kuchukua Leseni yangu baada ya leseni ya zamani kuisha na kutaka mpya ambayo nililipia siku 3 zilizopita. Ni huzuni sana leo nimetoka mbali na kutumia gharama kubwa hadi kufika Mkoani makao makuu hapa Moshi. Nimekaa foleni kuanzia saa 4 asbhi hadi saa saba.

Muda ukafika na Afisa muhusika akasema anaenda kula chakula. Saa nane mchana anarejea na kutuambia Wino wa ku print lessen na roller vimeisha turudi kuanzia jumatano wiki ijayo. Najiuliza uongozi husika haukujua wino unaisha? Mwenye Ofisi tangu saa nne anatudangaya tusubiri wakati anajua hakuna wino ana maanisha nn.

Lazima muelewe pia watu tunaacha kazi zetu kuja hapo kufanya Malipo na msionyeshe dharau za namna hiyo.

Wahusika tafadhali mzifanyie kazi kero za wananchi....Tunachoka pia
 
sawa wamekuelewa,watafanyia kazi jmatano ijayo usiende nenda jumatano ile ingne
 
TRA hawatoi Leseni Bali wanatoa TIN certificate (cheti cha utambulisho wa namba ya mlipakodi). Leseni zinatolewa Halmashauri za wilaya, miji na majiji. Kajitathmini Mkuu.
 
TRA hawatoi Leseni Bali wanatoa TIN certificate (cheti cha utambulisho wa namba ya mlipakodi). Leseni zinatolewa Halmashauri za wilaya, miji na majiji. Kajitathmini Mkuu.
Nina shaka na uelewa wako.....driving licence baada ya kulipia unachukua wapi?
 
Hivi bado kuna watu wapuuzi wa namna hiyo? Ningekuwa mimi angetoa wino hata kwenye pen anipe leseni yangu.

Watu kama hao ni wakung'olewa madarakani na wenyewe wajue adha ya wengine.

Pole sana, tafuta sehemu ulale kesho Urudi nyumbani
 
Nina shaka na uelewa wako.....driving licence baada ya kulipia unachukua wapi?
Sasa unaposema Leseni bila kuwa mahsusi ni Leseni gani unatutia shaka pia. Ndio maana nikakuchokoza makusudi ili uje umejipanga zaidi. Kwa sababu kuna Leseni ya biashara (Halmashauri), Leseni ya Kuendesha vyombo vya moto (driving licence), Motor vehicle Licence (Leseni ya Vyombo vya Moto). Jipange.
 


Ndg Kisinja.Ushauri wangu ungemtafuta Meneja wa Hapo TRA kuliko kuandika huku kwani ungeweza pata msaada au utatuzi wa kesi yako.Ni vizuri ukiona huduma hujaridhika nayo muone mkuu wa eneo husika kwani mlipa kodi anastahili huduma bora na ya haraka.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…