TPC yatumia Bilioni 1.5 kila mwaka kusaidia shughuli za kijamii ikiwamo elimu

Ndagullachrles

Senior Member
Jun 20, 2023
130
141
KIWANDA cha sukari cha TPC kilichopo mkoani Kilimanjaro,kinatumia kiasi cha sh Bilioni 1.5 kila mwaka kwa ajili ya kusaidia shughuli za kijamii kwa wananchi wanaoishi kuzunguka kiwanda hicho katika wilaya za moshi vijijini na Simanjiro mkoani Manyara.

Sehemu ya fedha hizo zinakwenda katika ufadhili wa wanafunzi wanaomaliza kidato cha sita na kushindwa kuendelea na maosmo ya elimu ya juu kutokana na familia zao kutokuwa na uwezo wa kulipia ada .

Chini ya Mpango huo,TPC kupitia Taasisi yake isiyo ya kiserikali ya Foundation for Community Transformation in Kilimanjaro(FTK),imefanikiwa kujenga shule mbili mpya za sekondari ikiwa ni mkakati wa kuwaondolea adha ya kusafiri umbali mrefu wanafunzi wanaotoka familia duni.

Mpango huo ulioanza mwaka 2012 hadi sasa umewezesha zaidi ya wanafunzi 1,000 wanaoishi kuzunguka kiwanda hicho katika wilaya ya Moshi Vijijini kunufaika na mpango huo ambao unatajwa kuwa utapandisha kiwngo cha ufaulu kwa wanafunzi hao.

Msimamizi wa Shirika hilo,Lazaro Urio, amesema hayo katika hafla ya kukabidhi Mabweni na Maktaba kwa shule ya Sekondari TPC, ambayo ni kitengo cha uwajibikaji kwa Jamii (CSR) cha Kiwanda cha Sukari TPC iliyofadhili ujenzi wa shule, mabweni na miradi ya maktaba.

“Kabla ya ujenzi wa shule hizo, wanafunzi wengi wao wakiwa ni watoto wadogo walilazimika kutembea umbali mrefu kufika shule zilizo nje ya eneo la TPC”, alibainisha na kuongeza, ndipo wazo la kuanzishwa kwa shule mbili za sekondari za TPC na Shule ya Sekondari ya Chewe katika eneo hilo ilianzishwa.

Urio amesema kuwa, baada ya kujengwa kwa shule hizo mbili, changamoto nyingine iliibuka ambapo amesema, safari hii wanafunzi wengi kutoka nje ya eneo la TPC walilazimika kutembea umbali wa kilomita 14 hadi 20 kwenda na kurudi kutoka katika shule hizo mbili.

"Ili kukabiliana na changamoto hiyo, FTK ilikuja na wazo lingine la kulipia usafiri wa wanafunzi kwa kukodisha mabasi, ambapo wazazi walialikwa kuchangia asilimia 50 ya gharama, lakini wengi hawakuweza kufanya hivyo kwa sababu mbalimbali", amesema.

Kwa mujibu kiongozi huyo, kufuatia changamoto hiyo mpya FTK ilikuja na wazo la ziada la kujenga bweni katika shule ya Sekondari ya TPC litakalohifadhi wanafunzi 64 waliokuwa wakitembea umbali mrefu kwenda na kurudi shule ya sekondari ya TPC.

“FTK iliamua kuwekeza katika shule ya Sekondari ya TPC kwa kujenga bweni jipya lenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 64 kwa gharama ya shilingi milioni 147, ambapo uongozi wa shule ulipewa jukumu la kuweka vitanda kwa ajili ya bweni hilo”, amesema Urio.

Kuhusu maktaba mpya ya shule hiyo, Urio amesema ujenzi wake umegharimu Sh milioni 126 na kwamba itajumuisha maabara ya kompyuta.

“Maktaba hii haina thamani hivyo nitoe rai kwa wadau mbalimbali kuungana na FTK kukusanya jumla ya Sh milioni 25 ili kumudu gharama za thamani zote zinazohitajika katika maktaba hiyo mpya”, amesema.

wanafunzi TPC.jpg
 
Back
Top Bottom