Toyota Allion Vs Toyota Premio ZZT 1.8L

Mapfa A

JF-Expert Member
Jan 9, 2015
250
258
Habari wakuu zangu!

Mimi ni kijana nimekuwa nikitamani kumiliki ka usafiri, Tamanio langu ilikuwa ni kumiliki Toyota Premio 2005 ZZT 1.8L yenye taaa tofauti na zile model za 2001-2004 .
Sasa nimejipapasa nimepata budget kama 13mil
Nimejaribu kutafuta premio yenye vigezo hivyo imekuwa Changamoto ila nimepita kwenye website ya SBI Motors japan nikaiona Toyota Allion 2003 ZZT 1.8 L ina milleage chache almost 24,000 km na ina hali nzuri sana na iko kwenye budget hiyo.

Ombi langu kwenu naomba ushauri wenu kati ya gari hizo mbili, Je niongezee budget nipate premio ya 2005 ambayo almost ni kama 16.5 mil au nichukue hiyo Allion 2003 yenye hali nzuri na milleage chache?

Je Fuel Consumption ,matengenezo na Spare parts kati ya hizo aina mbili za magari ukoje?

Naombeni ushauri wakuu wangu!

Nashukuru
 
Mambo ya budget huwa yanachangamoto Sana,kama ungekuwa mfuko wako uko vizuri ungenunua premio Tu ukaachana na allion.

kumbuka hata kama utaamuwa kuuza Kwa siku za baadae premio haitasumbua kivileee, jichange kidogo tena uvute hiyo premio
 
Hata allion pia mkuu ni gari kali sana. Nimeitumia iko vizuri, tofaut yake na hyo nyingine ni miaka tu. Ila premio na allion ni jamii moja na zote zinatumia mafuta vizuri sana/ ni economy.
Mi yangu ni ya 2004.
0655362575
Sema Allion watu hawaipendi kama Premio japo ni gari moja tu kwa maoni yangu with the same interiors finish! Allion ni nyeusi ndani while premio ni rangi ya mbao mbao
 
Sema Allion watu hawaipendi kama Premio japo ni gari moja tu kwa maoni yangu with the same interiors finish! Allion ni nyeusi ndani while premio ni rangi ya mbao mbao

Nashukuru mkuu!
Japo nimeshajitoa muhanga nimeshaagiza Allion ZZT 240 1.8L ya 2003 kupitia SBI Motors japo nimeambiwa kwa sasa usafiri ni changamoto.
 
Habari wakuu!

Nashukuru, Nimeshafanya maamuzi
Japo wengi walinishauri Toyota Premio ila nimefanya maamuzi na kuagiza Toyota Allion ZZT 240 1.8L ya 2003, binafsi imenivutia zaidi kwa kuwa interior na Exterior haina hata mchubuko na imetembea 24,000 km Tu! Ila premio nyingi niliona zinazoendana na budget yangu zimetembea km nyingi kuanzia 60,000 na kuendelea.

Nashukuru kwa maoni nitawapa mrejesho mzigo ukiingia.

Amina
 
Alion nzuri ikifika tia 17 inch rims itakaa poa sana tire za 215/45 itapendeza sana

Mkuu!
Yaani huo mautundu siyajui,
ndiyo mara ya kwanza kununua na kumiliki na gari.
Hizi ni baadhi ya picha zake.
IMG_3985.jpg

IMG_3984.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom