Tovuti za Vyuo Vikuu vya Umma Tanzania ni aibu wakiongozwa na UDOM na Nelson Mandela

saigilomagema

JF-Expert Member
Jun 5, 2015
4,577
7,117
Ndugu zangu watanzania wenzangu katembeleeni tovuti za vyuo vikuu vyetu vya umma anzia na UDOM, nenda Nelson Mandela uje uniambie kama utapata taarifa unazohitaji. Ndio maana watanzania wa kawaida wanawadharau wasomi wetu.

Unafungua tovuti ya UDOM ukitegemea upate programme lists, programme details, programme funding, programme duration, mode of delivery. Utategemea basi upate prospectus ya chuo, utaipata wapi imefichwa utafikiri ni confidential document wakati ile ni public document. Nafikiri kinachowapa kiburi ni kuwa hawahitaji marketing maana wanafunzi wanapelekewa na Serikali, na hawahitaji ushindani hata wasipopata wanafunzi mishahara yao iko palepale, posho zao ziko palepale ni kodi zetu, wamejibwetekea.

Lakini nenda tovuti ya vyuo vikuu vya Kenya hata kama ni cha umma kila unachohitaji utakipata. Kwa mfano katembelee tovuti ya Chuo kikuu cha Nairobi na kingine labda cha Kenyatta. Nelson Mandela ndiyo aibu, hivi Nelson Mandela inaisaidia nini nchi hii? Kile chuo kipelekewe wanafunzi wa undergraduate hakuna kinachofanyika pale zaidi ya kutafuna tu pesa za nchi hii. Tovuti yao ni aibu ukifungua tu jina la kozi ndiyo mwisho hakuna maelezo mengine tena.

Tovuti ya chuo cha kimataifa kama kile utafikiri ya zahanati ya kijiji kinachoweza kutengenezwa na kijana anayesomea cheti cha IT. Kwanza kwa mtindo huu chuo kitaingiaje katika World Ranking wakati wanaofanya ranking wanategemea kupata taarifa nyingi kutoka katika tovuti za vyuo husika?

NI AIBU KWA WASOMI HAWA.
 
Back
Top Bottom