Tovuti za baadhi ya Halimashauri Nchini zijitathimini na kuwajibika

Dalton elijah

JF-Expert Member
Jul 19, 2022
441
947
Ukienda kutazama tovuti za Baadhi ya wilaya nchini Tanzania utakuta taarifa za mwaka 2022, jambo ambalo linakatisha tamaa na kutoa taswira mbaya kwa halimashauru husika inawezekanaje mwaka 2025 unakutana na taarifa za mwaka 2022 hiyo inaonesha kuwa wasimamizi wa hizo tovuti hawatendi haki wala kuwajibika juu ya majukumu yao amabyo wamepangiwa

Mfano ukifanya upimaji wa kutembelea baadhi ya tovuti za halmashauri hazina taarifa mpya bali utakutana na taarifa za miaka ya nyuma hivyo kuzorotesha uhuru wa wananchi juu ufuatiliaji wa mambo yanayo endelea ndani ya halimashauri husika

Katika upande mwingine Taarifa au mawasiliano ya simu ambayo huchapishwa kwenye Tovuti za serikali hasa halimashauri nyingi hazipatikani hivyo wananchi hawana uwanda mpana wa kutoa taarifa endapo kutakuwa na changamoto katika eneo husika .Tunaomba serikali kuanza kuweka namba zinazopatikana kwenye tovuti ili kuwezesha wananchi na jamii husika kuwasilisha changamoto zinazo wakumbuka .

Je serikali ina mpango gani kuhusiana na kile ambacho kinaonekana katika tovuti za wilaya kushindwa kuakisi matarajio ya wananchi
 
Wilaya ya Nyasa website yao ni kichefuchefu. Wameshindwa kukielezea kwa mivuto kisiwa cha Londo, halafu wanategemea wapate watalii.

Ukitaka kujua kuwa serikali ya CCM imeajiri vilaza, basi tembelea website za serikali na taasisi zake, sio bunge wala ikulu, ni shaghala bagala
 
Ukienda kutazama tovuti za Baadhi ya wilaya nchini Tanzania utakuta taarifa za mwaka 2022, jambo ambalo linakatisha tamaa na kutoa taswira mbaya kwa halimashauru husika inawezekanaje mwaka 2025 unakutana na taarifa za mwaka 2022 hiyo inaonesha kuwa wasimamizi wa hizo tovuti hawatendi haki wala kuwajibika juu ya majukumu yao amabyo wamepangiwa

Mfano ukifanya upimaji wa kutembelea baadhi ya tovuti za halmashauri hazina taarifa mpya bali utakutana na taarifa za miaka ya nyuma hivyo kuzorotesha uhuru wa wananchi juu ufuatiliaji wa mambo yanayo endelea ndani ya halimashauri husika

Katika upande mwingine Taarifa au mawasiliano ya simu ambayo huchapishwa kwenye Tovuti za serikali hasa halimashauri nyingi hazipatikani hivyo wananchi hawana uwanda mpana wa kutoa taarifa endapo kutakuwa na changamoto katika eneo husika .Tunaomba serikali kuanza kuweka namba zinazopatikana kwenye tovuti ili kuwezesha wananchi na jamii husika kuwasilisha changamoto zinazo wakumbuka .

Je serikali ina mpango gani kuhusiana na kile ambacho kinaonekana katika tovuti za wilaya kushindwa kuakisi matarajio ya wananchi
Leo umeweka hoja mujarabu sana, halmashauri nyingi zimeoza
 
Back
Top Bottom