TORRENT jinsi jinsi INAVYOFANYA KAZI

its MalekoGJ

Member
Aug 27, 2020
28
68
"Torrents zinafanyaje kazi?" Ni swali ambalo wengi wamekuwa wakiuliza, hasa wale wanaodownload filamu, tamthilia, au programu kama Photoshop bila kulipia.

Katika uzi huu, nitakueleza kwa kina jinsi mfumo wa Peer-to-Peer (P2P) unavyofanya kazi kupitia Torrents.

Twende kazi! πŸ§΅πŸ‘‡

1/
Kwenye internet ya kawaida, unadownload faili kutoka kwa server moja kuu.

Mfano: Ukidownload Google Chrome, faili linatoka moja kwa moja kutoka kwa server za Google.

Tatizo? Kama server hiyo ikizimwa au ikipotea, faili halipatikani tena.

2/
Sasa fikiria umepakua faili kwenye Google Drive. Mtu mwingine anapotaka kudownload, lazima apate kutoka kwa akaunti yako.

Serikali ikiamua kuliondoa, wanaweza kulazimisha Google kufuta, na litapotea milele!

Hili ndilo tatizo la kutegemea server moja kuu.

3/
Hapo ndipo Torrents zinapokuja!

Badala ya kudownload kutoka kwa server moja, unadownload vipande vya faili kutoka kwa watu wengi kwa wakati mmoja.

Faili linahifadhiwa kwenye kompyuta za watu duniani kote, na kila mtu anachangia sehemu yake!

4/
Hii inajulikana kama Peer-to-Peer (P2P) Sharing.

Unadownload vipande vya faili kutoka kwa mamia ya watu tofauti. Na unapomaliza kudownload, unaweza kusaidia wengine kupata vipande walivyokosa.

Hii ndiyo nguvu ya ugatuaji (decentralization).

5/
Katika mfumo wa Torrent, kuna wahusika wawili muhimu:

πŸ”΅ Seeders – Wanaoshiriki faili (wanaupload).
πŸ”΄ Leechers – Wanaodownload faili kutoka kwa Seeders.

Ukidownload faili, unakuwa Leecher. Ukimaliza, unaweza kuwa Seeder ili kusaidia wengine.

6/
Lakini si kila mtu anataka kuwa Seeder!

πŸ‘‰ Watu wengi huzima seeding mara baada ya kudownload ili wasitumie data zao kusaidia wengine.

Lakini kama hakuna Seeders wa kutosha, basi hakuna faili la kudownload!

7/
Ili kutumia Torrent, unahitaji programu inayoitwa Torrent Client.

Maarufu zaidi ni:
βœ… uTorrent
βœ… BitTorrent
βœ… qBittorrent
βœ… Deluge

Hizi husaidia kudownload na kushiriki mafaili kupitia mfumo wa P2P.

8/
Kuna njia mbili za kupata mafaili ya Torrent:

🧲 Magnet Links
πŸ“‚ .torrent Files

Magnet Links huunganisha moja kwa moja kwenye Torrent Client bila kupakua faili ndogo la .torrent.

Mfano wa Magnet Link:
magnet:?xt=urn:btih:08ada5a7a6183aae1e09d831df674…

9/
.torrent Files ni faili dogo linalosaidia Torrent Client kupata Seeders na kuanza kudownload.

πŸ“Œ Magnet Links zimekuwa maarufu zaidi kwa sababu ni rahisi na hazihitaji kupakua faili ndogo kwanza.

10/
Wapi utapata mafaili ya Torrent?

βœ… The Pirate Bay
βœ… 1337x
βœ… YTS (YIFY)
βœ… LimeTorrents

Tovuti hizi hazihifadhi mafaili, bali zinatoa Magnet Links zinazowaunganisha na Seeders.

11/
🚫 Kutumia Torrent si haramu!

Lakini…

❌ Kudownload filamu mpya ya Marvel kupitia Torrent ni uharamia.
βœ”οΈ Kudownload Linux ISO kupitia Torrent ni halali kabisa.

Serikali zinapambana na Tovuti za Torrent kwa sababu wengi huzitumia kwa njia haramu.

12/
Watu wengi hujiuliza:

"Kwa nini serikali isiangushe server zote za Torrent?"

Jibu ni Torrent haina server moja kuu.

Ukidownload faili, unakuwa sehemu ya mfumo wa Torrent (unakuwa server pia).

13/
Kwa hiyo, ili kuzima Torrent, serikali inapaswa kuzima mamilioni ya kompyuta duniani kote – kitu ambacho hakiwezekani!

Hii ndiyo sababu Torrents ni ngumu kusimamishwa.

14/
Jinsi ya kuwa salama unapotumia Torrent:

βœ… Tumia VPN – Ili ISP (mtandao wako) isikufuatilie.
βœ… Soma comments kabla ya kudownload – Epuka mafaili yenye virusi.
βœ… Usitumie uTorrent toleo la kisasa – Limejaa matangazo na malware.

15/
Historia ya The Pirate Bay:

πŸ“Œ 2006 – DreamWorks ilitishia kuwafungulia mashitaka kwa kusambaza filamu zao.
πŸ“Œ 2009 – Waanzilishi wa Pirate Bay walifungwa jela na kupigwa faini kubwa.

Lakini tovuti iliendelea kuwepo kwa sababu haina server moja kuu!

16/
Mpaka leo, Pirate Bay imefungwa na kufunguliwa mara nyingi kwa majina tofauti tofauti.

Hii ni kwa sababu ugatuaji (decentralization) haufi kirahisi!

17/
βœ… Torrent ni mfumo wa kugawana mafaili kwa njia ya P2P bila kutegemea server moja kuu.
βœ… Ni vigumu kuzimwa kwa sababu kila mtu anayeshiriki faili anakuwa sehemu ya mfumo wa Torrent.
βœ… Si haramu, lakini inaweza kutumika kwa njia haramu.

18/
Je, ulikuwa unajua haya yote kuhusu Torrent?

Tuambie mawazo yako kwenye comments! πŸ‘‡πŸ½
 
Nimepata elimu nzuri sana hapa, you deserve a πŸ‘βœ”οΈ

Nakuomba uje na somo la VPN
 
ila kwa sasa izo site
βœ… The Pirate Bay
βœ… 1337x
βœ… LimeTorrents
nyingi hazipo update kwenye kudownload hapa, kwa sasa kweenye site zilizo kuwa update kudownload ni zile za direct download
 
Back
Top Bottom