Nimesikiliza wimbo wa mwana muziki mmoja nikaambiwa anaitwa Ney. Sikuwa namfaham nilisikilizishwa wimbo wake na mwenzangu mmoja. Ni wimbo wa kisiasa. Nlisikitika kuwa mwimbaji hakuwa mbunifu, hakuwa na uwezo mkubwa wa kuweza kufinyanga sanaa yake na hivyo Kujiepusha na madhara katika serikali hii.
Ni wangap walisoma kitabu cha Rosa Mistika? Ni wangapi wanajua kuwa mwandishi e.kezihalabi alizungumzia siasa katika namna ambayo ingekuwa ngumu sana kumkamata na kumweka ndani kwa madai ya uchochezi hasa katika awamu ile ya kwanza serikali ilikuwa sensitive sana.usingepata ushahidi katika maandishi yake. Lakini wenye akili walielewa. Na hata Nyerere alielewa kuwa amesemwa mle ndani.
Ulipata soma kitabu cha KAPTULA LA MARX? Mwandishi ni E. Kezihalabi pia. Hii ilikuwa kejeli kuhusiana na siasa za Ujamaa akimsema Mh J.K Nyerere miaka ile alikataza kitabu hiki Kisichapishwe.
Ebrahim Hussein alikuja na kitabu Chake cha Mashetani 1987. Alizungumza siasa katika hali ambayo msomaji unaweza changanyikiwa kama ambavyo inasemekana naye alikuja kuchanganyikiwa. Hii ilikuwa kazi ya Fasihi akizungumzia siasa.
Umesoma vitabu kama Morani, Kivuli kinaishi na Animal Farm? Sanaa ilifanya kazi yake kwa kiasi kikubwa sana Kuzungumzia siasa kwa Kificho ili kuepuka Udhamini. Lakini Kuna Mashairi mengi pia kama Malenga Wapya, Mashairi ya Chekacheka, Chungu Tamu n.k
Wanamuziki hawakuwa nyuma. Nani anaukumbuka wimbo wa Bomoa Leo tutajenga kesho? Wimbo huu ulipigwa marufuku. Nao ulikuwa ni kejeli.
Siku zote fasihi ina nafasi kubwa sana katika kuelimisha na kubirudisha na vijana wa sasa wengi wameshindwa kutambia hilo. Zaman walikuwa wanaifanya hiyo kazi kwa kutumia akili kubwa sana. Nawashauri wajipange wawe makini katika uchaguzi wa maneno yao na pia kutumia sanaa katika kazi zao. Ama sivyo tutajikuta tunawatafuta kama ambavyo mpaka leo hii hatujui Ben Saanane amepotelea wapi.
Kweli fasihi ina nafasi kubwa katika jamii yetu pia uchaguzi wa maneno na tafsida ni muhimu ila waqt mwingine kuna kujilipua kwa manufaa marehemu swalehe mwinamila kuna waqt aliimba "kuimba sana mwisho wake utakufa lofa "watu aaah wakamjengea nyumba dodoma. Dk remmy alijilipua ala timing haikuwa nzuri alipoimba mambo kwa soksi radio tanzania hawakuurekodi wimbo ule lakini leo si jambo la ajabu kiongozi mkubwa kuhamasisha umma matumizi ya vifungashio ambavyo havijapigwa marufuku (kondomu )ila vijana wanamaliza kabisa hakuna tafsida yaani nyeupe wala hawapepesi midomo.
Sio kwa kizazi hiki,hiki ni kizazi cha makavu laivu,ukizingua unapewa zako za uso,hakuna ku sugar coat,wananchi wenyewe wengi vichwa ngumu ukiweka tafsida na mafumbo mengi watakaokuelewa wachache.
Sio kwa kizazi hiki,hiki ni kizazi cha makavu laivu,ukizingua unapewa zako za uso,hakuna ku sugar coat,wananchi wenyewe wengi vichwa ngumu ukiweka tafsida na mafumbo mengi watakaokuelewa wachache.