Tofauti ya mavazi wanayovaa raia wa Rwanda, Uganda na Tanzania kwenye harusi

Money Stunna

JF-Expert Member
Aug 9, 2011
13,053
6,294
img_3330.jpg


AFPGetty-482944423.jpg


Haya ni mavazi wanayovaa wanyarwanda kwenye harusi bila kujali kabila la mtu, harusi zote za wanyarwanda huvaa hivyo. Napenda sana mavazi yao.





Ugandan-Wedding.jpg


Haya ni mavazi ya waganda kwenye harusi bila kujali kabila wote huvaa hivi kwenye harusi na napenda sana mavazi yao.

Sasa twende kwa Tanzania:

Tanzania ni vurugu kila mtu anajivalia vazi lake analojisikia, hakuna vazi maalumu labda kwenye kitchen party ndio watu angalau hushona sare sare lakini hakuna vazi maalumu. Wengine huvaa ata vimini kila mtu anatoka vile anajisikia.

Kwa tanzania wasimamizi peke yao ndio hushona sare, raia wengine wanakuwa huru kuvaa watakavyo tofauti na nchi za Uganda na Rwanda. Huwezi ukavaa tu vimini vyako kwenye harusi, hizo nguo uvaliwa club.

Sorry sitoweka picha za Tanzania sababu hakuna vazi maalumu la nchi. Mkiwa na vazi maalumu nitarudi kuweka picha. Samahani kwa hilo.
 
Mkuu upo sahihi kwa Tanzania,kuna siku bidada alivaa kimini hicho balaa(hajachuchumaa chupi inaonekana).Ukumbi mzima uliamishia macho kwake.
 
Tanzania ni vurugu kila mtu anajivalia vazi lake analojisikia,hakuna vazi maalumu,labda kwenye kitchen party ndio watu angalau ushona sare sare lakin hakuna vazi maalumu.

wengine uvaa ata vimini kila mtu anatoka vile anajisikia.

Kwa tanzania wasimamizi pekeyao ndio ushona sare,raia wengine wanakuwa huru kuvaa watakavyo,tofauti na nchi za Uganda na Rwanda uwezi ukavaa tu vimini vyako kwenye harusi hizo nguo uvaliwa club.

Sorry sitoweka picha za Tanzania sababu hakuna vazi maalumu la nchi.Mkiwa na vazi maalumu nitarudi kuweka picha,samahani kwa ilo hakuna picha kwa Tanzania. BYE................
Sio tu Rwanda na uganda pekee mbona warundi wanavaaga hivyo hivyo tena siotu kwenye sherehe /shughuri Bali hata makasani wanavaa jiridhishe kwa ku Fanya tafiti ya kutosha ndugu mhariri
 
Vazi la Rwanda linaitwa "Mshanana" ni maalumu kwa shughuli zozote za harusi au sherehe yeyote ya kitaifa ama kimataifa. Jamaa wako stricted kiaina maana hawana Uhuru wa kuishi wanavyotaka.

Kwa Bongo mambo ni nyooso..kila mtu anaamua kuvaa anachoona kinampendeza..mavazi ya Rwanda kuna wengine wakivaa wanakuwa kama Wacambodia au wavetnam jinsi yanavyowachoresha.
 
Nabaki na Tanzania yangu kama tulivyo makabila tofauti na tunaishi kwa upendo basi na kwenye tafrija nyingi tunatokea tofauti tunafurahia tofauti zetu na tunaijenga nchi yetu nyie wapuuzi mnaokuja kuomba pa kulala ndio mnaokuja na kelele kama hizo.
 
Back
Top Bottom