John Magongwe
Member
- Jan 4, 2024
- 60
- 86
Tofauti ya Matoleo na Sadaka na Utoaji Wake
Kumekuwa na mijadala mbalimbali kuhusu neno sadaka. Wapo wanaoita sadaka na wapo wanaotumia neno matoleo. Matoleo ni neno la ujumla, linalomaanisha aidha sadaka, au michango.
Neno matoleo linatokana na neno kutoa. Hivyo chochote kile mtu anachokitoa kwa minajili ya Mungu kinaitwa matoleo. Neno hilo limejikita katika maeneo mawili makubwa, yaani sadaka na michango.
Sadaka ni matoleo yanayolenga moja kwa moja madhabahu. Sadaka ni matoleo ya siri.
Sadaka haipaswi kuwa kitu cha kuonyesha mbele za watu, bali inapaswa iwe siri ya mtu na Mungu wake. Bwana wetu Yesu alitufundisha:
Mathayo 6:2 “Basi wewe utoapo sadaka, usipige panda mbele yako, kama wanafiki wafanyavyo katika masinagogi na njiani, ili watukuzwe na watu”.
3 Amin, nawaambieni, wamekwisha kupata thawabu yao.
Bali wewe utoapo sadaka, hata mkono wako wa kushoto usijue ufanyalo mkono wako wa kuume; 4 sadaka yako iwe kwa siri; na Baba yako aonaye sirini atakujazi”.
Michango inaweza kuwa ni kwa ajili ya kujenga au kukarabati kanisa, kununua vyombo vya mziki vya kanisa, na huduma zingine za kanisa. Michango ni matoleo ya waziwazi, hadharani.
Mfano wa matoleo ya Anania na Safira Kwa mfano, yale matoleo ambayo Anania na Safira mkewe walitoa baada ya kuuza viwanja na kuleta thamani yake chini ya miguu ya mtume Petro (Matendo 5:1-11), hayakuwa siri, bali lilikuwa ni jambo linalowekwa wazi kwa wote.
Matoleo yote (iwe sadaka au michango) yana thawabu kubwa mbele za Mungu, kama yakitolewa kwa nia njema na dhamiri njema, na kulingana na Neno la Mungu, na Mungu anayaangalia sana.
Ukiahidi au ukipanga kumtolea Mungu kitu, basi hakikisha unatimiza kama ulivyoahidi au ulivyopanga pasipo kupunguza hata kidogo, ili isiwe kwako dhambi kama ilivyokuwa kwa Anania na Safira mkewe, ambao walimdanganya Roho Mtakatifu kwa matoleo yao (Matendo 5:1-11).
Utoaji wa sadaka
Utoaji, uwe wa sadaka au wa kitu kingine chochote, ni wajibu wa kila muumini. Mtu ambaye si mtoaji bado hana badiliko la kweli ndani yake, na wala Mungu hayupo ndani yake.
Tunatoa sadaka kwa sababu Mungu naye ni Mtoaji. Vyote tunavyonufaika navyo ni yeye ametupatia bure, bila gharama yo yote. Je, kwa nini Mungu awe mtoaji na sisi tuwe watoaji.
Ni kwa sababu tumeumbwa kwa sura na mfano wake (Mwanzo 1:26).
Kama mtu hatoi, maana yake ni kwamba ule mfano wa Uungu ndani yake haupo. Ni kwa sababu Mungu sifa yake kuu ni utoaji. Ametoa uzima bure, ametoa maisha bure. Zaidi sana ametupa uzima wa milele bure, kupitia kumtoa mwanae wa pekee (Yohana 3:16). Na mambo mengine mengi. Hivyo, na sisi ni lazima tuwe kama yeye, ndivyo maandiko yanavyotuambia (Mathayo 5:48): “Basi ninyi mtakuwa wakamilifu, kama Baba yenu wa mbinguni alivyo mkamilifu”.
Tufahamu kuwa kutoa ni wajibu zaidi kuliko agizo. Mtu anayejua wajibu wake, hakumbushwi, halazimishwi, wala hasukumwi. Anatimiza wajibu wake kwa sababu anajua pia ni kwa faida yake.
Ukiona utoaji ni sheria ngumu kwako, kwamba unaona uchungu kumtolea Mungu, au unaona kama unafilisika, au unaonewa au unadhulumiwa, wahi kutafuta msaada kutoka kwa Bwana. Mlilie.
Mwambie aiondoe hiyo roho ndani yako, kwa sababu ndiyo roho ile ile iliyokuwa ndani ya Kaini. Kaini aliona kumtolea Mungu sehemu ya kwanza ya vitu vyake vizuri ni hasara kubwa. Na kwa vile alisukumwa na sheria ya utoaji, akalazimika kumtolea Mungu sehemu hafifu ya sadaka zake, na hivyo zikakataliwa.
Hivi, kwa mfano, Mungu anayekupa pumzi na maisha bure, unaonaje uchungu kumtolea sehemu 1 ya kumi tu, na sehemu 9 zilizosalia ubaki nazo. Huoni kuna shida hapo, kama unaona uchungu kwa hicho kidogo.
Mungu unayekanyaga ardhi yake bure, unayevuta hewa yake bure tangu umezaliwa, unayefurahia jua lake bure bila kulipia, na wakati huo huo unawalipa shirika la umeme fedha nyingi kwa kukupatia mwanga kidogo wakati wa usiku.
Huyo Mungu akupaye hayo yote, unamwonea uchungu na hata kumwibia, na ukiambiwa kuhusu kumtolea unaona unafilisiwa na kudhulumiwa, utaachaje kuwa kama Kaini. Moyo wako hauwezi kuwa kwa Mungu kamwe, haijalishi utakuwa unaomba sana, huo utakuwa ni unafiki.
Tumeona kuwa matoleo ni kitu cho chote kinachotolewa kwa minajili ya kumtumikia Mungu. Tumeona pia tofauti kati ya matoleo na sadaka. Kwamba, matoleo yako katika makundi makubwa mawili. Kundi moja ni sadaka, ambayo hutolewa kwa siri tu, bila mtu mwingine kufahamu, bali mtoaji na Mungu pekee (Mathayo 6:3-4). Kundi lingine ni michango ya kuimarisha kanisa, ambayo hutolewa waziwazi au hata kwa siri, kulingana na mazingira yaliyopo ya uchangiaji.
Kwa kufahamu tofauti kati ya matoleo na sadaka, usikwepe kumtolea Mungu, tena ifanye kuwa ni wajibu, na siyo agizo wala amri. Kumbuka kuwa kuna madhara ya kutomtolea Mungu. Madhara hayo yapo katika Mathayo 25:41-46.