To my African Comrades (Kama hatuwezi kusimamia lolote, tunaweza kusimamia Nchi)

Logikos

JF-Expert Member
Feb 26, 2014
15,074
23,703
Preamble: Binafsi naamini Free market na Competition ndio inaleta Huduma Bora na Bei rahisi kutokana na kwamba watu wanashindana kugombania wateja. Ingawa kuna mambo ya Huduma naamini kabisa Serikali / State ni muhimu kujikita kinagaubaga.., Mengine yote luxurious hatuna haja ya kuweka Kodi zetu huko tuachie watu binafsi 100 percent (wala hatuna haja ya PPPs tunaweza kuwakodisha infrastructure)

From Self Reliance to Total Dependency
Ila imetokea Kasumba moja kwamba Waafrika / Raia hawawezi. Nikichukulia Case Study ya Kenya na Management ya Airport yao (Jambo ambalo ingawa wanapiga kelele litapita) Adani atapewa na ukiuliza kwanini wasifanye wenyewe utajibiwa hawawezi..., Sasa Adani amewezaje ? (Hii Kampuni ambayo ipo linked na Prime Minister wa India) iliweza kupewa kuendesha Airport Sita za India (Bila experience yoyote). Yaani waliondoa Kipengele cha Previous Experience required na Adani akapewa.... Anazo contracts za kuendesha Airport Saba nyingine kwa mpaka miaka 50....; Sasa kama Adani ameweza tena bila kuwa na Prior Experience sisi tunashindwa vipi ? Badala ya kumpa mtu the whole nine yards kwanini tusitoe lease fupi fupi kwa vitu tofauti ? Mfano Maduka, Hotels, n.k. kwa Wato tofauti in open transparent tenders ?

Kumbuka kulikuwa na levy ambayo ilikuwa inakusanywa kwenye kile Ticket na huduma za pale Airport kwa miaka mingi sana ili mwisho wa siku Airport iweze kupanuliwa sasa hizo pesa zilizokusanywa huenda ikawa zawadi ya Ajaye Kufanya, Eti sababu sisi Hatuwezi...

Case Study ya TTCL: Sio mbaya kipindi hiki ambacho mawasiliano ni muhimu sana kuwepo na hata Kampuni moja ya UMMA ikishindana na Kampuni nyingine binafsi, ili hata wakitaka kufanya cartels na kupandisha bei Kampuni ya UMMA itajitahidi kuwa kimbilio la watu (affordability) lakini utasikia watu wanasema uza yote UMMA hauwezi.., sasa unajiuliza mbona HALOTEL imetokea huko Vietnam na kufika mpaka huku ? Kwanini TTCL isitumie Economic Power yake iweze kuvuka bahari na kufika nje ?

Samsung Case Study: Hii Samsung inayopeperusha bendera kila mahali ingawa ni Private ila ina government backing, iliweza kupewa Tender zote kubwa na serikali na kwa upendeleo ndio maana ikaweza kukua, ni kwamba imeweza kuchanja mbuga kutokana na government backing..., Ndio hivyo hivyo kwa Adani na kupewa Upendeleo na Prime Minister na kupewa Tender za Airports kuendesha without even Prior Experience

NBC Case Study: Hii Benki tuliibinafsisha kitambo sana na mpaka sasa tuna kama 30 percent pekee.., sasa cha kujiuliza miaka yote hiyo tumebinafsisha lakini mpaka leo haina hata Tawi lolote nje ya nchi na hata ndani ya nchi ni Benki ya Tatu yaani inazidiwa na NMB na CRDB

In the World of Automation and Technology (Blockchain ) We do not Need Manpower / Expertise as Before
Dunia ya Sasa ya Teknolojia ambapo ufuatiliaji umekuwa rahisi kusema kwamba tunashindwa kusimamia kitu ni kujitoa ufahamu au kama hatuwezi nadhani kulikuwa hakuna haja ya kuondoa Ukoloni.., Na kama kweli hatuwezi kwanini tusiajiri experts na kuwapa goals ili wafanye na tuwalipe

Way Forward:
Lazima tuwe na Stake kwenye Commanding Height of the Country Economy Hususan Sehemu za Huduma au zile ambazo ni Natural Monopolies (Nishati), Usafiri, Mawasiliano, Banking na vyote hivi vifanyike kwenye Open Market..... Na cha kujiuliza ni Kwanini Hatuwezi..., Sio sababu hatuwezi tunamuita Jirani aje afanye..., Inabidi tuweze ili sisi ndio twende tukawafanyie Majirani....
 
@Mods Naomba Heading Isomeke hivi

To my African Comrades (Kama hatuwezi kusimamia lolote, tunawezaje kusimamia Nchi)​

 
Hmmm

Kujenga taifa la watu ambalo linayonasibu ya kuhama kutoka kwenye akili na ufahamu wa 'jamii asili' na kuupeleka kwenye akili na ufahamu wa 'jamii dunia' ni jambo tata kama siyo gumu--labda wenye kuzungumza haya mawili, kwa lugha ya kiingereza, wangeyataja haya kwa dhana kana 'complexities' na vile vile 'complicated'--complex if not complicated state of affairs vs collective/self determination...

Sasa, utata ama ugumu; vyote viwili vinatokana na uwezo, vipawa na ujuzi wa kiakili, katika mtu mmoja mmoja ama makundi ya watu, kwenye kukabiliana na hali ilivyo.

Hili ndilo jambo linalohusiana na 'Elimu'... Shughuli ya 'kuwaelimisha wanajamii' ili watambue na kutambua yanayopaswa kufanywa/kutendeka kwa ajili ya 'mazingira muafaka'--mazingira muafaka ya mwenendo wa utamaduni na ustawi wao'.

Haya maneno mawili 'Utamaduni' na 'Ustawi'; kiufundi, yanapitiliza dhana rahisi za 'jamii na kuelimishana'--Utamaduni na Ustawi ni shughuli inayogusa nasibu na misimamo ya Kiutu na Kiroho ya makundi ya watu.

Sasa, kuna utata na ugumu hata katika 'jamii dunia'; utata na ugumu wenye kukadirisha muktadha akilifu wa uwezo, vipawa na ujuzi wa kiakili wenye basi kubayanishwa kuwa ni 'mushkeli'. Vivyo hivyo, Kuna namna yake ya kulibayanisha hili kwa kusudi la kuamsha utambuzi wa kiutu na kiroho katika mtu/wanajamii--mambo kana kusema: ulimwengu wa biashara huria na masoko una 'mema na mabaya' yake pia...

'Mema na mabaya' ya ulimwengu wa biashara huria na masoko, kiutu na utamaduni, ndiyo pia huhitaji jamvi la 'aliyelala asiamushwe...'; vile vile mambo ya kiufundi kuhusiana na 'kula vizuri na vipofu'...

Kwa hivyo mambo kama 'aliyelala asiamushwe' na pia 'kula vizuri na vipofu', kiufundi ndiyo 'kompromaizi za kiutu na kiroho' za jamii dunia/utamaduni globali ya kileo, 2024.

Ndiyo, kuna utundu na ufundi wa kumeneji utata ama ugumu katika ulimwengu wa kileo; jambo ambalo linawezekana kwa kitu/jambo la ujuzi--kitu tunachoweza kutaja kama 'Ufikirifu Mifumo'. Mambo ya huu ujuzi wa ufikirifu mifumo una 'nidhamu' na pia nasibu ya 'muktadha akilifu wa 'fremukazi' ya UONO wa namna yake--'Uono Mifumo'...

Uono na Ufikirifu Mifumo, hata katika domaini ya wasomi wengi wa leo, ni 'fumbo la imani'--japo mtu yeyote mwenye nasibu ya uono na ufikirifu mifumo ni rahisi kubaini usomi uliotamalaki ni 'elimu mashudu'; watu wanalishwa mafikara, fafanuzi na tafsiri za mambo zilizo mushkeli huku wao wakiamini/kusadiki mamlaka ya taasisi zao za visomo na elimu--kusadiki/kuamini kwa hadhi na daraja ya 'ufikirifu pofu wa kimakundi'....

Ni 'Ufikirifu pofu wa kimakundi' unaozidi kuponza na kuzamisha jahazi--jahazi hata la 'jamii asili' zinazonasibishwa na 'UTAIFA MCHANGA'...

Kwa hivyo kiufundi, 'jamii asili' huhitaji mageuzi ya kiufahamu kwa ajili ya utayari na uweza ili 'Kujijenga Kitaifa'.

Mageuzi ya Kiufahamu ni shughuli zaidi ya 'mambo ya maelimishano ya kimadarasa' na 'Uhitimu'...

'Mambo ya Maelimishano ya Kimadarasa' yananasibu ya 'Uraibu wa Teja wa Mafanikio Binafsi'--teja wa utu usio na moyo wa kujali mafanikio ya pamoja ila 'mafanikio binafsi' ilivyo ni mambo ya kujipendelea na 'Maslahi Binafsi'--pepo ya Mabwege...

Mambo ya kujipendelea na Maslahi binafsi ndilo suala mtambuka kuhusiana na 'Maadili' na mwenendo wa UTU katika Kujichagulia namna ya mapenzi ya kuishi, maisha na uisho... Hili ndilo kwa mfano, ni khasa mzizi wa 'Utata' wa udhamirifu wa 'maendeleo Binafsi dhidi ya Maendeleo ya Umma'...

'Uraibu wa Teja wa Mafanikio Binafsi'--Uteja ulivyo ni muktadha wa mtu mmoja na udhamirifu wake wa furaha hata kwa gharama ya wengine 'wanaojitafuta/waliozubaa/waliolala'--kujifaidisha na hali ya hawa ikibidi. Hili ndilo changamoto ya ugumu wa kuukadirisha muktadha akilifu wa 'maadili na miiko' ya utendaji wa mwanajamii ili kutangamanisha 'mafanikio binafsi' na 'mafanikio ya Umma'...

BASI, kwa jamii kisomoni, tuseme jamii ya Watanzania kwa mfano, topografu moja ya kiuono na ufikirifu mifumo kuhusiana na kubayanisha 'utendaji/kujichagulia/Matokeo' ni jambo tunaloweza kulimbonisha kwa usahihi wa katikati kama 'Ushamba wa Kutojielewa ilivyobora'. Ashkum 'ushamba' si tusi, ni tu ile hali ya mtu kuwa mgeni na jambo fulani ambalo tayari linamzunguka-- na kumuumbua mbele ya jicho la mwenyekujua ilivyobora; ama kubidi kumuinua ili ananufaike na 'mambo ya nyakati' katika sura/hadhi ya 'utendaji/Kujichagulia/Kulala'... Labda tutohoe neno la lugha ya kiingereza kwa ajili ya maana ya ushamba: 'Unaivu'... Kutokana na neno naivety...

Unaivu ni nasibu ya watu wa namna zote tu, wasomi na hata wasio wasomi katika 'jamii asili' ama pia 'jamii mabadilikoni' -- kama ilivyo kwa 'Taifa la Watanzania'. Japo kwa akili ya kawaida wanajamii hudhani 'uzoefu huondoa unaivu wa mambo', kwamba 'Ushamba Mzigo'; Udhamirifu wa Maarifa na Maarifu ya mambo ndiyo chachu ya kweli ya mageuzi/mabadiliko ya Kijamii. Hata kwa kudhamiria 'kawaida' fulani ya mazoea ya kiutamaduni katika mseto wanajamii bado jambo hili linawezakuwa linagubikwa na 'unaivu kumbaizi'...

Taifa la Watanzania, bado lina idadi ndogo ya wanajamii wanaoweza kukadirika kama 'Watu wa Mwangaza' ili kuleta nuru ya maendeleo ya kweli ya UTU na si vitu. Ulimwengu wa vitu ni jamvi la 'majaribu ya Kiutu' ambavyo wanajamii wanaweza kuingia vishawishi kulingana na dhamiri zao mbovu na mawazo na basi kuingia kwenye 'mtego wa shetani'--kuzitumikia nafsi zao pofu kiroho... Basi ndiyo kuna muktadha akilifu wa ushetani ama umalaika katika nasibu ya jamii mabadilikoni--inategemea na mtu/mwanajamii anakina gani katika 'utashi wake wa kiroho'...

Kwa hivyo kuna jambo kama 'Utashi wa Kiroho'--hili jambo ndiyo nyeti kuliko nyeti zote za hadaa za walimwengu; kuanzia mapana ya siasa-uchumi hata nchi na tawala...

Inaweza kuwa ni shauri lisilolakawaida kusisitiza hapa, matatizo yote ya kijamii yanawezakutokomezwa--kutokomezwa kwa kina na kheri ya kudumu kwa vitovu utu na kujichagulia vyenye chaji bora ya 'utashi wa kiroho'-- 'SIYO USOMI' wala 'MAENDELEO KWA KUIGA VITU/MAMBO'. Maendeleo kwa kuiga ni 'Ushamba'--ushamba usiyo na tofauti ya 'kuvaa nguo za kuazima zisizositiri maungo'...

Kwa hivyo, wanajamii wa taifa la watanzania--walio wengi, ikiwa bado wanajitafuta kwa wakati huu ama mwingine wowote wanaweza kuwa naivu sana kiasi cha kusadiki maendeleo yanaletwa na 'mtu' badala ya 'taasisi'. Wanakuwa vipofu kung'amua ya kwamba taasisi ndiyo muktadha akilifu wa utendaji wa kimifumo unaotafuta usahihi wa Kufufuka kutoka kwenye Mauti ya Kiroho...

Japo kwa mfano, kuweka kikatiba ya uhuru wa mtu kuchagua na kuchaguliwa ili awe nayo dhamana ya uongozi, uongozi wa umma, haina maana kwamba 'mtu yeyote' anaweza kufanya maajabu kwa kuwa 'yeye ni yeye'; maajabu ya mageuzi ya kijamii, mageuzi yenye kheri kweli kweli, yanawezekana kwa muktadha akilifu wa 'Utaasisi'. Jamii ya Watanzania ina/itapata mageuzi na mabadiliko haya pale watendaji kadhaa pamoja na wanajamii wenyewe watakapoanza kutenda kwa koherensia ya vitendo/utendaji ilivyo ni 'Taasisi'--si 'sinema' ya mtu mmoja / 'taasisi mfu' katika ushabiki na mkumbo wa mawazo mushkeli...

Mifano yote ya 'visomo kesi' ulioyoileta inaleta hesabu rahisi ya uwepo 'pengo la Utaasisi' katika ushabiki na mkumbo wa mawazo mushkeli; huenda inamapotoshi yake kulingana na ugeni wa mtu mmoja kwa zile 'kweli za kiroho' zinazoathiri utendaji wa kitaasisi na mifumo. Pasipo Utashi wa kiroho, koherensia ya Utendaji, na Maslahi ya Kweli ya Taifa, maslahi yenye kitovu cha UTU KWELI KWELI, hata 'mifano ya duniani' nayo ni 'Kiini Macho'...

Ujamaa na kujitegemea unawezekana; unawezekana kwa idadi muafaka ya wanajamii na watendaji wa kiserikali wenye Elimu 2.0 na Elimu 3.0, mtu yeyote asidanganyike na visomo empirikali vya walimwengu--huenda huu unakuja kuwezekana hapa Tanzania na Afrika; haijalishi 'hatuna mfano wa huu kokote hata katika ulimwengu wa leo', tuseme 2024.​
 
Back
Top Bottom