TMA: Kutakuwa na Upepo Mkali unaozidi Kilomita 40 kwa siku 3 mfululizo nchini

Wild Flower

JF-Expert Member
Jul 20, 2023
325
674
Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa taarifa Septemba 1, 2024 kuwa kuna uwezekano wa kutokea kwa upepo mkali unaozidi kilomita 40 kwa siku tatu mfululizo kuanzia Septemba 1 hadi Septemba 3, 2024

Taarifa hiyo imesema kuwa Athari zinazoweza kujitokeza ni kuathirika na kughairishwa kwa baadhi ya shughuli za baharini na kuharibika kwa miundombinu ya bahari, hivyo ni vyema kuchukua tahadhari

Imetaja maeneo yatakayo athiriwa baadhi ya maeneo ya ukanda wa Pwani ya kusini mwa bahari ya hindi katika mikoa ya Lindi na Mtwara, baadhi ya maeneo ya kusini mwa ziwa Tanganyika mikoa ya Rukwa na Katavi, maeneo ya ukanda wa Pwani ya kaskazini mwa bahari ya hindi katika mikoa ya Dar es salaam, Tanga, Pwani(ikijumuisha visiwa vya Mafia), pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba

 
Back
Top Bottom