Resilience
JF-Expert Member
- Jan 4, 2023
- 1,032
- 4,733
Aliposema Mbowe ilionekana upinzani; aliposema Kitima ikaonekana Udini; akasema Warioba ikaonekana uzee unasumbua; akisimama Dr. Slaa akaambiwa alihongwa; Tundu Lisu hakujibiwa kabisa kama ilivyo kwa Lipumba na wazalendo wengine.
Sasa imekuja taasisi ambayo inaundwa na watu wa vyama vyote; dini zote, pande zote za Muungano na rangi tofauti. Taasisi hii inaitwa TLS ( ikumbukwe wapo wazanzibari ambao ni wanachama ndo maana nasema pande zote za Muungano). Taasisi hii ambayo baadhi ya Mawaziri, Wabunge, viongozi waandamizi serikali ni wanachama imesema kwamba MKATABA WA BANDARI UNA DOSARI KUBWA SANA.
Kutokana na uchambuzi wa taasisi hii ambayo asilimia kubwa ya wanasheria hata wa CCM niwanachama inamaanisha kwamba wanasheria wote wa TLS kwa kauli moja wanasema mkataba mbovu. Yawezekana hata AG naye ameunganishwa kwenye hili tamko la kitaaluma kama naye ni mwanachama.
Swali, tunatokaje hapa? Ni kwa namna gani wanasheria watusaidia kusema tena kwamba mkataba hauna matobo? Kwamba leo kwa umoja wao wametamka mbele ya Dunia kwa lugha ya Kiingereza kwamba mkataba una shida....wanachama wanaopingana na hii kauli ya TLS chini ya Sungusia ni wapi? Tuache uchawa na tusiwachanganye wananchi; ni mwanasheria gani anasema mkataba ni mzuri?
Ningependa sana pasiwepo na ukimya; wasiokubaliana na msimamo wa TLS watoke adharani waseme tuwasikie. Wakikaa kimya means wanajua ukweli na ukweli ndio huu wa chama chao.