Mitandao ya simu pamoja na kurahisisha mawasiliano imekuwa njia rahisi sana ya kutumia na kupokea pesa, na kukiwa na jambo la dharula basi muamala ya simu inatoa suluhu ya haraka sana.
Kwangu imekuwa tofauti, ilikuwa tarehe 22/12/2024, saa 2:38 asubuhi, nilienda kwa wakala kutoa pesa niliyotumiwa kwa ajili ya matibabu ya ndugu yangu, (115,000), lakini bahati mbaya wakala hakuwa na cash na mimi sikumuuliza (kwani mara nyingi ninatoa pesa kwake, is hiyo nilipofika tu nilifanya mchakato wa kutoa pesa)
Baada ya dakika 3 akaniambia kwa muda huo haha cash, na ana safari kwa hiyo nirudishe muamala, (hapo ndipo tatizo lilipoanzia), niliingia kwenye menyu ya Mixx by Yas,na kuingia namba 6 (juhudumie) Kisha nikazuia muamala wangu.
Nikaambiwa nisubiri masaa 24 pesa ingerudi kwenye account yangu, na wakala aliwapigia kusisitiza kurejeshwa kwa muamala huo, wakamwambia wakala asubiri kupigwa. Hawakumpigia, na Wala pesa haikurudi kwangu japo kwa wakala pia waliizuia! (I.e HAIPO kwa wakala Wala kwangu)
Kila nikiwapigia simu wanasema "tatizo lako linashughulikiwa" na sasa ni siku ya saba,sijalipiwa pesa ya matibabu ya mgonjwa, na hakuna dalili za kunirudishia pesa!
Je, naweza kuwashtaki tigo/Yas kwa hiki walichonifanyia? Maana pesa yangu naipigia magoti kwa hawa tigo/Yas! Na Wala hawajali kabisa!i