TIGOPESA/Mixx by Yas huu ni wizi? Au kutojali wateja wenu?

Theunknown

JF-Expert Member
Dec 30, 2017
295
320
Mitandao ya simu pamoja na kurahisisha mawasiliano imekuwa njia rahisi sana ya kutumia na kupokea pesa, na kukiwa na jambo la dharula basi muamala ya simu inatoa suluhu ya haraka sana.
Kwangu imekuwa tofauti, ilikuwa tarehe 22/12/2024, saa 2:38 asubuhi, nilienda kwa wakala kutoa pesa niliyotumiwa kwa ajili ya matibabu ya ndugu yangu, (115,000), lakini bahati mbaya wakala hakuwa na cash na mimi sikumuuliza (kwani mara nyingi ninatoa pesa kwake, is hiyo nilipofika tu nilifanya mchakato wa kutoa pesa)
Baada ya dakika 3 akaniambia kwa muda huo haha cash, na ana safari kwa hiyo nirudishe muamala, (hapo ndipo tatizo lilipoanzia), niliingia kwenye menyu ya Mixx by Yas,na kuingia namba 6 (juhudumie) Kisha nikazuia muamala wangu.
Nikaambiwa nisubiri masaa 24 pesa ingerudi kwenye account yangu, na wakala aliwapigia kusisitiza kurejeshwa kwa muamala huo, wakamwambia wakala asubiri kupigwa. Hawakumpigia, na Wala pesa haikurudi kwangu japo kwa wakala pia waliizuia! (I.e HAIPO kwa wakala Wala kwangu)
Kila nikiwapigia simu wanasema "tatizo lako linashughulikiwa" na sasa ni siku ya saba,sijalipiwa pesa ya matibabu ya mgonjwa, na hakuna dalili za kunirudishia pesa!

Je, naweza kuwashtaki tigo/Yas kwa hiki walichonifanyia? Maana pesa yangu naipigia magoti kwa hawa tigo/Yas! Na Wala hawajali kabisa!i
 
Sio peke yako mkuu. Nami nilikutana naa tatizo kwenye mtandao huu nisiouamini kwa sasa. Nilienda kwa wakala kutoa pesa pesa ikakatwa kwenda kwa wakala lakini mimi sikupata sms wala wakala hakupata sms ya kupokea pesa. Nikawapigia has Yas wakasema mtandao wao wa mix uko chini kwa hivyo nimwambie wakala atazame salio. Wakala hakuona ongezeko la pesa na akiwapigia hawapokei na muamalq aukurudi kwangu pamoja na jitihada za kifanya hivyo. Sasa inaenda wiki ya nne nimeamua kutumia laini yao kwa kupiga na kupokea simu tu. Wamenitia hasara hawa watu nahisi kuna jambo sio bure na customer service yao mbovu sana unaweza kupiga simu yao hawapokei hadi unahisi kukata tamaa kutumia laini yao...daaa
 
Mimi Jana nimekumbana nalo tatizo nlihamisha hela kutoka tigo pesa/yas kwenda Voda miamala haitoki inasitishwa nlikwazika Sana. Nliwapigia eananiambia Wana tatizo kwa pande wap nisubiri saa 24 wakati hapo nini siku 2 nasumbuka nliwatukana nikakata cm maana ukihamisha Voda kwenda tigo wap hela wanaipokea chap unaiona.
 
Tigo wanakwambia tatizo Lako tumeliwasilisha. Unasubiri majibu inakua kimya hata wiki mbili. Ukipiga tena wanakwambia tatizo Lako tumeliwasilisha.....hivyo mpaka nimewaacha
 
Back
Top Bottom