Tigo Customers Service usiku mnaenda Disco?

Nazjaz

JF-Expert Member
Jan 20, 2011
7,725
9,050
Wahudumu wenu wamelala. Receiver wameweka pembeni, namba zote zina onekana ziko busy, nimeweka simu sikioni kwa zaidi ya Saa mzima nina shida nahitaji msaada, nashangaa huduma kwa wateja Saa nane usikuvhii wako busy. Ni rahisi kumpata mtoa huduma wa Tigo mchana kuliko usiku,
#tigo_timu_lalafofo
 
Naunga mkono hoja, kuanzia saa 6 usiku ukiwa na dharura na unahitaji msaada huenda ukaishia kusikilizishwa muziki tu; jamaa wamesinzia.

Kisha ukiwasikiliza behind the scenes kwenye matangazo yao wanasema wanatoa huduma 24 hours, huu ni ulaghai uliopitiliza.
 

Hadi kunakucha sijapata huduma.
 
Tigo niajirini na mimi, night shift nalala kama maiti, receiver naweka kando
 
Nilinunua bando lao GB 10 kwa mwezi ila cha ajabu sikuweza kutumia hata MB 50 kutokana na mtandao wao kuwa down.

Nikawapigia simu wakanambia niongeze salio maana salio langu ni kidogo sana na ndio maana inapelekea mtandao kusoma low hivi, haikuniingia akilini ila sikubisha nikafanya walivyonielekeza

Baada ya kufanya hivyo mtandao ndio kwanza unasoma "E" hadi mwezi unaisha bila mafanikio. Na laini yangu ni 4G Cha kushangaza hata ikiwa inasoma 4G, kudownload tu picha ya KB 200 unaweza ukachukua hata DK 10

Kwa sasa nimetupa line yao kule coz sipendagi stress kabisa
 
Tangu customer care department iwe outsourced kwa wale wahindi wa spanco bpo/ison morali ya wafanyakazi wa call center ya tigo ipo chini sana manake wanalipwa mshahara mdogo sana.
Kima cha chini kwa sekta ya mawasiliano kwa mujibu wa sheria kinapaswa kuwa si chini ya laki tano lakini kwa sasa wanalipwa laki mbili tu.

Sasa hapo unategemea nini kama sio poor service.

Na hili tatizo halipo tigo tu lipo kwenye karibia makampuni yote ya simu manake walifanya kosa kubwa kubinafsisha kitengo cha call center kwa makampuni mengine ambayo yanaendesha kibiashara zaidi.

Zamani wakati wafanyakazi wa call center walipokuwa wanaajiriwa direct na makampuni husika ya simu morali +commitment ya wafanyakazi ilikuwa juu kutokana na mishahara mizuri pamoja na kuongezewa allowances nyinginezo mfano night shift allowance.
 
Sisi huku Moro kidogo alihamdulilah inafungua chap
 
Well said mkuu.
 
Niko dar Ila sina tofauti na mtu alieko porini. Tigo imekuwa ovyo sana kwenye Internet
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…