MALCOM LUMUMBA
JF-Expert Member
- Jul 26, 2012
- 21,035
- 64,851
THE BASHITE EFFECT:
Nchini Tanzania kuvunja muungano ni jambo rahisi sana kuliko kumfukuza kazi Makonda.
Uongozi ni sayansi,
Sayansi ni muunganiko wa kanuni mbalimbali za kitaalamu zilizothibitishwa kitaalamu katika nyanja husika. Hivyo basi kama unataka kukokotoa hesabu za magazijuto ni lazima ufuate kanuni zake za kitaalamu ambazo zimethibitishwa kitaalamu.
Basi uongozi hauna tofauti kabisa na kukokotoa hesabu za magazijuto, ukifuata kanuni lazima ufanikiwe na usipofuata lazima utafeli tu. Lakini tofauti kabisa na sayansi nyingine za dunia hii, UONGOZI WA KISIASA ni sayansi ngumu sana kuliko zote kwasababu ili kupata majibu yake haitegemei pekee utashi na mchango wa kiongozi wa kisiasa, bali pia utashi na mchango wa watawaliwa.
Sasa ili kuhakikisha hili linafanyika sisi kama watanzania tuliamua kutengeneza Sheria, Kanuni na Taratibu za kiutawala. Bahati mbaya sana leo hii tumeamua kuzikanyaga kwa makusudi kwa kutumia msemo wa "kunyoosha nchi" bila kufikiria mbali kwamba uongozi ni sayansi ambayo ni lazima isomwe vizuri na kanuni zake zifuatwe ndiyo nchi huweza kwenda mbele. Hapa haitajalisha kwamba wewe una nia njema na nchi au una uchungu sana na nchi. Usipofuata kanuni na taraibu zilizowekwa na hata kukufikisha wewe madarakani lazima utaingia tu kwenye shimo "You are doomed to fail".
Historia inatufundisha kwamba hii imekuwa ndiyo Sheria Kuu ya Uongozi tokea miaka 5000 iliyopita (Kabla ya Kristo)ambapo ustaarabu wa kwanza wa binadamu ulianza kujengeka huko Mesapotamia. Kibaya zaidi na kinachoogopesha ni kwamba dunia imebadilika sana hivyo kuongezea kanuni mpya sana katika sayansi ya uongozi. Dunia ya wakina Mfalme Koreshi wa Umedi, Mfalme Charlamagne wa Roma, Mfalme Napoleon wa Ufaransa hadi Kaiza Wilhelm wa Ujerumani ni tofauti sana na dunia ya wakina Kagame wa Rwanda na Magufuli wa Tanzania. Hii dunia ya karne ya ishirini na moja ni mbaya sana kwasababu hakuna tendo utafanya au neno utasema katika uongozi lisilje kuwa na madhara mazuri au mabaya kwa wananchi wako na dunia nzima kwa ujumla: Huu ndiyo utandawazi wenyewe.
Sasa hayo ya juu ni kujenga msingi tu, kilichonileta leo hii hapa ni hili swali moja tu:
Hivi inawezekanaje vitendo vya muhuni mmoja anayejiita Paul Makonda viweze kuhatarisha na kutishia mustakabali mzima wa mfumo utawala wa nchi hii bila hata viongozi wa nchi kustuka kwa namna yoyote ile ? Ndiyo, huyu ni muhuni kwasababu mpaka sasa serikali imeshamkana mara tatu mbele ya ummah kwa vitendo vyake viovu ambavyo vilihatarisha usalama na amani ya nchi hii. Watanzania ni watu wasahaulifu sana lakini hebu tuweke kumbukumbu zetu sawa juu ya huyu mtu kukanwa na serikali ya Jamhuri ya Muungano:
Mosi, alivamia kituo cha habari kwa kutumia vyombo vya dola na kuwateka waandishi wa habari huku nchi nzima na dunia ikishuhudia. Mwitikio wa kwanza wa Serikali ulikuwa ni kwenda kulaani kitendo hicho na kusema siyo cha Serikali bali cha mtu huyu kiongozi binafsi. Aliyefanya hii kazi ni Waziri wa Habari, Sanaa na Michezo wa wakati huo Ndugu Nape Nnauye. Lakini baada ya lile tukio Nape alitumbuliwa na likatokea songombingo la yeye kutishiwa silaha ya moto na moja ya askari wa usalama ambaye inasemekana alifanya hiyo chini ya maelekezo ya huyu Mhuni anayejiita Paul Makonda. Baada ya lile tukio Raisi wa nchi Mzee Magufuli alikemea vyombo vya habari huku akimkana tena Makonda na kusema hivi "Waandishi wa habari wanaripoti vitu vya kichochezi kwenye magazeti utadhani Serikali ndiyo ilibariki kitendo hicho (Cha Nape kutishiwa Bastola)"
Pili, aliingiza makontena yenye bidhaa zake binafsi kinyume kabisa na sheria za nchi na akakataa kulipa kodi huku akizitishia mamlaka za Serikali akiwemo Waziri wa fedha na mipango kwamba atawashitaki kwa Raisi wa nchi kwa kosa la kuwa wazalendo kwa nchi yao. Hili kwenye utawala tunaita ni utovu wa nidhamu wa hali ya juu mno "First Degree Insubordination". Sakata likaendelea Raisi wa nchi akainuka na kumkana kwa mara ya pili na kusema kwamba zile siyo bidhaa za Serikali hivyo Mkuu wa Mkoa ni nani hata asilipe kodi. Hivi umewahi kujiuliza madhara ya muda mrefu ya hili songo-mbingo kiutawala ?? (Nategemea waungwana wote washaelewa)
Tatu, juzi tena serikali imemkana kwa mara ya tatu mbele ya nchi na dunia nzima kwa ujumla kwamba kile kitendo cha kuwasaka mashoga ni matakwa yake yeye kama Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam na siyo msimamo wa Serikali. Nahisi yeye na washauri wake walishindwa kutofautisha kisheria kati ya "Vitendo vya ushoga" na "Kuwa shoga" au kwa lugha ya kiingereza tunasema he failed miserabaly to draw a distinction between "Homosexual acts such as having carnal knowledge of the member of the same sex group against the order of nature" and "Being a homosexual". Je, vitendo vya ushoga ni makosa kisheria ?? NDIYO ni makosa kisheria, tofauti kabisa na maadili ya watanzania na Sheria haitambui ndoa ya jinsia moja. Hivyo tutaendelea kuvikemea hivyo vitendo kwa nguvu zote: Lakini Je, unahisi mbinu ambazo Paul Makonda alizitumia katika kuwasaka hawa watu zilikuwa ni sahihi ?? (Hili nakuachia ujibu mwenyewe)
Hayo yote niliyoyataja hapo juu yanatupeleka kwenye Kanuni mbili za Kisheria na Kiutawala kama ifuatavyo:
1. Kanuni ya Ministerial Responsibility
2. Kanuni ya State Responsibility
A: MINISTERIAL RESPONSIBILITY
Hii ni moja kati ya kanuni muhimu sana ya Kikatiba ambayo hujenga msingi wa utawala wa nchi. Kanuni hii inataka Serikali nzima kuwajibika kwenye Bunge kwa vitendo vyote ambavyo imevifanya. Hivyo kitendo cha kiongozi moja Serikali "The Executive" akifanya jambo bovu kiutendaji basi inayowajibishwa ni Serikali yote (Collective Responsibility). Au mara nyingine kanuni hii humwajibisha waziri husika katika kila majukumu anayofanya ndani ya wizara yake "Individual Ministerial Responsibility". Pengine kueleweshana zaidi Serikali haiwajibiki kwa Bunge bali wananchi, ila inaenda kwa Bunge kwasababu bunge huwakilisha wananchi wote na kwasababu kitendo cha demokrasia ya moja kwa moja "Direct Democracy" hakiwezekani kwenye nchi ya watu zaidi ya milioni 50. Japo zamani huko Ugiriki ya kale sehemu kama Athens viongozi wote wa Serikali waliwajibika moja kwa moja mbele ya Ummah kwasababu idadi ya wananchi haikuwa kubwa sana kama ilivyo leo hii.
Upande wa pili, kutokana na kukua na kukomaa kwa utawala hapa duniani, hii kanuni haifanyi kazi tu kwa mawaziri. Hivyo jina lisikuchanganye kabisa. Hii hufanya kazi kwa kila kiongozi wa Serikali ambaye anapokea amri kutoka kwenye muhimuli wa Serikali "The Executive". Hivyo basi inagusa hadi matendo ya Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya hadi Wakurugenzi. Katiba ya Jamhuri wa Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, kwenye Ibara ya 35(1) inasema kwamba kila kiongozi wa Serikali atafanya kazi kwa niaba ya Raisi"
Sasa hivi wakina Dr Mahiga na Dr Kilangi wanavyotuambia kwamba yale anayofanya Paul Makonda siyo matakwa ya Serikali huku Serikali inanyamaza kimya bila kumchukulia hatua yoyote ile, wanaamaanisha kwamba Dar es Salaam inatawaliwa kwa Sheria tofauti na zile za sehemu nyingine au Dar es Salaam ni nchi huru ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kama ambayo Vatican iko huru ndani ya Italy ??? Huu ni upumbavu wa Karne. Katika sheria za utawala ili kuonesha kwamba Serikali haijabariki vitendo vya viongozi wake basi ni lazima ichukue hatua ya kumfukuza au kumpa adhabu. Marehemu Mzee Kingunge akiwa Waziri alishawahi kukataa waziwazi kuunga mkono Serikali ya Mzee Nyererena kilichofuata ni Chama na Serikali kumwambia ajiuzuru. Mifano iko mingi sana kuanzia wakina Mzee Emilio Mzena, Mzee Ali Hassan Mwinyi na Mzee Lowassa.
Hawa wazee ilibidi wafanye hivi kutunza heshima ya Serikali, Sasa huyu Makonda ambaye amekanwa wazi wazi lakini hafanywi kitu tutaaminije kwamba anachofanya hakina baraka za serikali ?? Hivi mmetuona sisi watanzania ni wajinga sana eeh ??
Makonda anahatarisha usalama wa nchi pamoja na uongozi wake maana mwisho wa siku jumba likianguka lawama zote atakayebeba ni Raisi Magufuli kwasababu viongozi wote wanafanya kazi kwa niaba yake kama Katiba isemavyo. Huyu Makonda asipochukuliwa hatua stahiki mapema basi atakuwa ni chanzo kikubwa sana cha anguko la Serikali ya Magufuli.
B: STATE RESPONSIBILITY
Hii ni kanuni ya kwenye Sheria za Kimataifa, Sayansi ya Siasa na Diplomasia inayosema kwamba Serikali ya nchi fulani itawajibishwa kwa vitendo viovu vya mawakala wake vilivyofanywa dhidi ya nchi nyingine, mali zake au makampuni yake. Hapa mawakala wanaweza kuwa Mawaziri, Wanajeshi au Majasusi ili mradi tu wawe kwenye nafasi ya kuiwakilisha nchi yao na maslahi yake (The Principle of Imputability or Immutability). Nitoe mfano Mzuri tu mwaka 1988 majasusi wa Libya walilipua ndege ya Pan Am Flight 103 na kusababisha vifo vya wasafiri 243 na wahudumu 16. Libya alikana kuhusika lakini Ghadaffi aliambiwa kwamba kama Serikali yake haijahusika basi lazima ionyeshe ushirikiano katika kuwakamata hao majasusi waliofanya hilo tukio.
Upande mwingine mwaka 1985 Serikali ya Ufaransa iliingia kwenye mtafaruku baada ya kulipua meli ya New Zealand (The Raibow Warrior) ambayo ilikuwa inaende kuzuia majaribio ya Silaha za kinyuklia za Ufaransa ambayo yalikuwa yanahatarisha mazingira. Serikali ya Ufaransa ilikana kutokuhusika na tukio hivyo kuwakabidhi majasusi waliohusika na kuwapa adhabu ya kifungo cha miaka kumi pamoja na kulipa faini kwasababu walifanya kitu ambacho Serikali haikuwaagiza. Ina maana Serikali ya Ufaransa ingekataa uhusika bila kuchukua hatua yoyote ile ingeonekana kwamba imehusika moja kwa moja na kile kitendo.
Turudi kwa Paul Makonda: Hivi mngefanya nini kama huyu jamaa angeanza kuwakamata na kuwafanyia vurugu raia wa kigeni ambao wanasemekana ni mashoga waliofunga ndoa wakiwa huko nchini kwao na kuja hapa Tanzania kikazi au kiutalii ?? Sitetei Ushoga lakini hebu tujiulize vizuri kuhusu hili suala. Hivi mataifa ya nje yangetuelewa ? Au tungefanya kama ambavyo Waziri Hamis Kigwangalah alipendekeza "Machoko Wasiingine nchini kwetu na tuwazuie huko Airport". Kwanini tusifuate Approach ya Urusi kuhusina na Ushoga. "Not recoginised, Not segregated, Un-Violable as long as You don't Ask and Don't tell" Kuna ugumu gani hapa ?? Au mnaogopa ??
Tukiangalia kwa mapana mpaka sasa inaonyesha ni dhahiri Paul Makonda ni kichaa aliyepewa Rungu, ana nguvu kubwa sana kisiasa na anaweza kufanya jambo lolote lile hapa nchini. Kama huyu mtu hatafungwa lijamu mapema huko mbeleni anaweza kufanya vitu vya ajabu mno. Hivi ingetokea kwamba kawadhuru raia wa nje na hata kupoteza maisha unategemea nchi itakuwa kwenye hali gani ??
Au hata huko mbeleni akafanya kitu chochote kibaya dhidi ya makampuni au raia wa kigeni (Maana Hashindwi kabisa) tena hasa kipindi hichi ambacho Chama cha Mapinduzi (CCM) kinaamini kwamba kinapambana na mitandao ya Kibepari ndani ya nchi unategemea nchi itakuwa kwenye nafasi gani ?? Au bado hamuanini tu, katika hili ninalosema ?? Hebu ngoja niwape mifano ya mwisho na tufunge ukurasa:
Mfano wa kwanza, Mzee Edward Lowassa alikuwa ni mwanasiasa mwenye nguvu sana hapa nchini, mwaka 2014 akiwa Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi ya Bunge aliwahi kuongea Kauli ambayo ilitaka kuiingiza nchi kwenye matatizo. Kuhusu Malawi alitishia na kusema kwamba "Liwalo na liwe" huku huo haukuwa msimamo wa nchi na mwenye mamlaka ya kusema hivyo ni Amiri Jeshi Mkuu pekee. Mzee Jakaya alipoenda kwenye kikao cha SADC aliikana ile Kauli kwa kusema kwamba yeye ndiyo Amiri jeshi hivyo Lowassa apuuzwe. Kama Malawi ingekuwa ni nchi yenye nguvu kama Ethiopia sidhani kama tungekuwa kwenye mahusiano mazuri mpaka leo hii.
Mfano wa pili, Vita ya kwanza ya dunia iliyoua mamilioni ya watu ilianzishwa na kijana mdogo, mwenye akili mbovu na fupi kama Paul Makonda. Gavrilo Princip alikuwa ni mwanaharakati anayepigania Uhuru lakini kwenye genge lao la Kigaidi al maarufu kama The Black Hand walidanganyana wamuue mwanamfalme wa Austria Hungary bwana Ferdinand. Walivyomuua Serikali ya Bosnia ikajidai kutaka kukana kuhusika huku ikiwalinda hawa magaidi kama ambavyo Serikali yetu inamlinda huyu muhuni. Kilichotokea ni kwamba nchi nzima ilivamiwa na mataifa makubwa kisa kigenge cha wahuni wachache tu.
NB: Unaweza kusema nimewaza mbali au upumbavu na kubeza ninachosema hapa lakini kama mtu alidiriki kumfanyia shambulio mtu mzalendo, mzee, Makamu wa Raisi Mstaafu, Waziri Mkuu Mstaafu, Jaji Mstaafu na Mwanasheria Mkuu Mstaafu Jaji Joseph Sinde Warioba uandhani kuna kitu ambacho mtu wa namna hii anaweza asikifanye ??? Tena kama aliyafanya haya wakati hana ushawishi wowote ule, je leo hii alivyokuwa na baraka za Raisi wa nchi kufanya anachokitaka atashindwa kufanya lolote hapa nchini ???
Mtu wa namna hii hashindwi kukudhuru hata wewe uliyemweka hapo. Hili nalo huamini kabisa ?
Hebu nikufungulie ukurasa wa kumbukumbu. Mtu wa kwanza kumweka Paul Makonda kwenye ramani ya siasa za nchi hii ni Raisi Jakaya Mrisho Kikwete. Ambaye mbali na kuonywa sana kuhusu uadilifu wa huyu mhuni alienda mbele bila kufikiria makosa aliyofanya dhidi ya Mzee Warioba na kumpa ukuu wa wilaya. Raisi Jakaya kama wewe ulivyo sasa alihisi anatukomoa watanzania, lakini Mungu siyo athumani haikupita hata muda huyu Paul Makonda kwa kulinda tumbo lake akaifanyia vibaya sana familia ya Mzee Kikwete (Wanaofuatilia siasa za nchi wanaelewa namaanisha nini). Hivi mtu kama huyu unadhani atashindwa kukugeuka wewe kulinda tumbo lake ? Au unahisi alichokifanya ulikuwa ni uzalendo ? MAJUTO NI MJUKUU WA UZEENI, AMBAYE HUKUGANDA MPAKA KUFA.
Juzi pale Mlimani Raisi umesema tuwavumilie hawa vijana kwasababu damu inachemka lakini nia yao ni njema tu, Sisi tunasema hivi:
Mosi, Nchi inaongozwa kwa kanuni na taratibu tena tunategemea hawa vijana wasomi ndiyo wawe mstari wa mbele kutii sheria.
Pili, Tuwavumilie mpaka lini wakati kila siku matendo yao ndiyo yanaongezekana kasi ??
Tatu, Je tuwavumilie hata pale ambapo wanatishia Usalama na mustakabali wa taifa hili ambalo umelipokea likiwa na utulivu ??
Nne, Hawa vijana wako wakivuruga nchi yetu na kuumiza maelfu ya watanzaia wewe kama Raisi utakubali kubebe wajibu ??