TFF yawakuta na hatia ya upangaji matokeo na kuwafungia maisha Yusuph Kitumbo na Ulimboka Mwakingwe kujihusisha na soka

Influenza

JF-Expert Member
Jul 1, 2018
1,500
3,698
Shirikisho la Soka la Tanzania (TFF) limewafungia kujihusisha na mpira Mwenyekiti wa Kitayosce FC inayoshiriki Ligi daraja la Kwanza (Championship), Yusuph Kitumbo na kocha wa soka, Ulimboka Mwakingwe baada ya kutiwa hatiani kwa kosa la upangaji wa matokeo

Wamekutwa na hatia ya upangaji wa matokeo kwenye mchezo wa Championship wa Aprili 29, 2023 kati ya Fountain Gate FC dhidi ya Kitayosce.

E95323F9-C14F-43DC-9EA3-769FF08E1F34.jpeg

Pia soma > Kwa hili TFF hamtoibeba tena Kitayose >> Yusuph Kitumbo mkurugenzi KITAYOSCE Anayetoa rushwa michezoni kwa kurubuni wachezaji. TFF Chukua hatua

Klabu ya Fountain Gate ilituma barua ya malalamiko kwa Bodi ya Ligi Kuu kuhusiana na tuhuma za rushwa na upangaji matokeo zikimuhusisha Mwakingwe na Kitumbo
5F6CA906-C247-44D8-B645-B756FDF457A7.jpeg


Sehemu ya sauti ambazo inadaiwa kuwa zimetumika kama ushahidi katika tuhuma hizo..


 
Uyo Ulimboka matukio yake yanajirudia, mwaka 2010 alisha wahi kukaa mahabusu pale Morogoro baada ya kukamatwa na polisi Kwa kosa la kwenda Manungu kumpelekea fedha Kipa wa Mtibwa sugar Shaban Kado Ili golkipa Kado aachie Magoli kwenye mechi ya Simba na Mtibwa pale Manungu.

Pesa izo shilingi 300,000/= alizokamatwa nazo zilitoka kwenye uongozi wa Simba.

Baada ya kufikishwa polisi alidai pesa alikua akimpelekea Shaban Kado Kipa wa Mtibwa na alidai alikua anakwenda kumlipa Kipa uyo deni lake.

Hata ivyo Shaban Kado alikataa kumdai Ulimboka na kueleza pesa izo zilikua Kwaajili ya hongo Ili Simba ipate ushindi pale Manungu.
 
Uyo Ulimboka matukio yake yanajirudia, mwaka 2010 alisha wahi kukaa mahabusu pale Morogoro baada ya kukamatwa na polisi Kwa kosa la kwenda Manungu...
Ifikie wakati huyu Ulimboka Mwakingwe apelekwe tu Takukuru, ili akataje mtandao wote unaomtumia kuhonga wachezaji wa timu pinzani kwa lengo ovu la kupanga matokeo.

Kumfungia tu maisha haitoshi.
 
Yaan inakarbia kupanda ligikuu anaanza ujinga, au ndo zao kupanga matokea that's why Yuko nafasi hio.
 
kuanzia ligi kuu hadi ligi ya chini kunarushwa sana huyu Ulimboka ni mzoefu, tungekuwa na waandishi kama wale wa Italy tungeshuhudia madudu mengi ila waandishi wengi wamejikita kwenye bahasha ndio maana haya mambo yanafichwa
 
Back
Top Bottom