MwananchiOG
JF-Expert Member
- Apr 4, 2023
- 1,528
- 3,243
Uwanja wa Mkapa upo katika ukarabati, jambo lililopelekea baadhi ya mechi hususan hizi mechi za hatua ya awali kutoruhusiwa kutumia uwanja wa Mkapa mpaka hatua ya makundi ambapo vilabu ndipo huruhusiwa kutumia uwanja wa mkapa. Tumeshuhudia vilabu kama Yanga na Azam vikitumia viwanja vingine. Endapo TFF itaruhusu baadhi ya yimu kuutumia uwanja huo, itakuwa jambo la aibu kwa mpira wa Tanzania.