Tenda ya kuingiza mafuta nchini yadaiwa kutolewa kwa 'uswahiba', mmiliki wa Super Markets za TSN atajwa

Ambakucha

JF-Expert Member
Aug 16, 2019
305
501
Wadau habari zenu? Poleni na majukumu ya siku. Zipo habari kwamba, tenda ya kuingiza mafuta nchini ambayo wamepewa baadhi ya wafanyabiashara wachache nchini ambao wana uswahiba na kigogo wa wizara hiyo.

Kwa mujibu wa mtoa habari mmoja wa ndani ya wizara hiyo, kigogo huyo amewapa tenda wafanyabiashara hao maswahiba wake ambao baadhi yao hawana mtaji mkubwa wa kumudu kuingiza bidhaa hiyo nchini.

Mfanyabiashara ambaye ametajwa moja kwa moja na chanzo hicho kuwa, hana mtaji wa kutosha wa kuingiza bidhaa hiyo nchini ni mmiliki wa Super Market za TSN (Tanzania Sisi Nyumbani), Bwana Faruku.

“Ana pesa ndiyo, lakini siyo ya kumudu kuingiza mafuta nchini Tanzania. Huu utoaji tenda ni wa uswahiba sana. Kama kweli Serikali ina nia ya kupunguza bei ya bidhaa hiyo, watoe tenda kwa wafanyabiashara wenye mitaji mikubwa, la sivyo hakutakuwa na mabadiliko ya bei ya bidhaa hiyo,” kilisema chanzo hicho.

Siku za karibuni kumekuwa na mjadala mkubwa kuhusu otoaji wa tenda hiyo ambapo, baadhi ya wadau wanataka tenda itolewe kwa kila mfanyabiashara mkubwa na siyo kwa wachache kama ilivyo sasa ambapo habari zinadai ni wafanyabiashara watano tu tena wanahisiwa kukosa sifa.

Baadhi ya wadau wakiwemo wachambuzi wa mambo ya uchumi waliishauri Serikali kutoa uhuru kwa kila mfanyabiashara mwenye sifa, kuruhusiwa kuingiza bidhaa hiyo nchini ili kuthibiti bei kupanda kama ilivyo kwa bidhaa nyiingine ambazo bei zake zinadhibitiwa kwa uhuru wa wafanyabiashara wengi kuruhusiwa kuingiza bidhaa nchini.

Walisema kuwa, hawaoni sababu ya serikali kung’ang’ania kuingiza bidhaa hiyo kupitia Bulk Procurement ilhali wako wafanyabiashara wengi wenye nia, uwezo na sababu ya kuisaidia serikali ambayo kupitia wakala wake ndiyo watakuwa wakipokea mafuta hayo na kuangalia ubora wake kama unakidhi au la!

Kufuatia bei ya mafuta kupaa nchini na kusababisha bidhaa mbalimbali kupanda ikiwemo nauli za mabasi, Rais wa Tanzania, mama Samia Suluhu Hassan alisema Serikali itakuwa ikitoa Bilioni 100 kila mwezi katika kupunguza ushuru wa uingizaji wa mafuta nchini lengo likiwa kuifanya bidhaa hiyo isipande bei. Zoezi hilo lilianza mara moja na ndiyo iliifikisha bei ya Petroli kuwa Shilingi 3,000 kwa lita.

Hata hivyo, licha ya Serikali kutoa kiasi hicho cha pesa na bei ya mafuta kuwa Shilingi 3,000, bado bei ya bidhaa nchini ipo juu huku bei ya unga ikilalamikiwa kila kukicha kwamba, hadi Julai mwaka huu, kilo moja ya unga imefikia Tsh. 1,800 kutoka bei ya Tsh. 1,000 Februari mwaka huu.

Jana, Waziri wa Nishati, Januari Makamba alipotafutwa kwa njia ya simu ili kuulizwa kuhusu madai ya tenda kutolewa kwa uswahiba, hakupatikana hewani.
 
Tuache kulialia, hii dunia ni mali ya mamafia na kila kitu huenda kimafiamafia tu, the only choice is you to be the part of it otherwise you will collapse.
Unataka kuhalalisha nn tena? Ingekua hivyo Raisi angevunja, Jeshi, polisi, takukuru, usalama. Maana hao hiyo ndio kazi yao.
 
Kwa mujibu wa mtoa habari mmoja wa ndani ya wizara hiyo, kigogo huyo amewapa tenda wafanyabiashara hao maswahiba wake ambao baadhi yao hawana mtaji mkubwa wa kumudu kuingiza bidhaa hiyo nchini.
Huyu kigogo lazima atakuwa "yuleyule anaenyooshewa" vidole kila uchwao!
Na hizi 'tabia' zipo katika damu yao na kamwe hawezi kuacha upigaji!
 
Kipi kimeshindikana kwa TPDC yetu kupewa uwezo (mkopo toka benki zetu) wa kununua mafuta haya toka Urusi ambako bei yake ni nafuu sana? Rais Museveni wa Uganda kakubaliwa na Urusi kuanza kuletewa mafuta hayo. January Makamba kwa nini hataki kufanya hivyo?
 
Sasa huyo Taifa gas Distribution Manager ana akili za kuona mbali?
 
Wadau habari zenu? Poleni na majukumu ya siku. Zipo habari kwamba, tenda ya kuingiza mafuta nchini ambayo wamepewa baadhi ya wafanyabiashara wachache nchini ambao wana uswahiba na kigogo wa wizara hiyo.

Kwa mujibu wa mtoa habari mmoja wa ndani ya wizara hiyo, kigogo huyo amewapa tenda wafanyabiashara hao maswahiba wake ambao baadhi yao hawana mtaji mkubwa wa kumudu kuingiza bidhaa hiyo nchini.

Mfanyabiashara ambaye ametajwa moja kwa moja na chanzo hicho kuwa, hana mtaji wa kutosha wa kuingiza bidhaa hiyo nchini ni mmiliki wa Super Market za TSN (Tanzania Sisi Nyumbani), Bwana Faruku.

“Ana pesa ndiyo, lakini siyo ya kumudu kuingiza mafuta nchini Tanzania. Huu utoaji tenda ni wa uswahiba sana. Kama kweli Serikali ina nia ya kupunguza bei ya bidhaa hiyo, watoe tenda kwa wafanyabiashara wenye mitaji mikubwa, la sivyo hakutakuwa na mabadiliko ya bei ya bidhaa hiyo,” kilisema chanzo hicho.

Siku za karibuni kumekuwa na mjadala mkubwa kuhusu otoaji wa tenda hiyo ambapo, baadhi ya wadau wanataka tenda itolewe kwa kila mfanyabiashara mkubwa na siyo kwa wachache kama ilivyo sasa ambapo habari zinadai ni wafanyabiashara watano tu tena wanahisiwa kukosa sifa.

Baadhi ya wadau wakiwemo wachambuzi wa mambo ya uchumi waliishauri Serikali kutoa uhuru kwa kila mfanyabiashara mwenye sifa, kuruhusiwa kuingiza bidhaa hiyo nchini ili kuthibiti bei kupanda kama ilivyo kwa bidhaa nyiingine ambazo bei zake zinadhibitiwa kwa uhuru wa wafanyabiashara wengi kuruhusiwa kuingiza bidhaa nchini.

Walisema kuwa, hawaoni sababu ya serikali kung’ang’ania kuingiza bidhaa hiyo kupitia Bulk Procurement ilhali wako wafanyabiashara wengi wenye nia, uwezo na sababu ya kuisaidia serikali ambayo kupitia wakala wake ndiyo watakuwa wakipokea mafuta hayo na kuangalia ubora wake kama unakidhi au la!

Kufuatia bei ya mafuta kupaa nchini na kusababisha bidhaa mbalimbali kupanda ikiwemo nauli za mabasi, Rais wa Tanzania, mama Samia Suluhu Hassan alisema Serikali itakuwa ikitoa Bilioni 100 kila mwezi katika kupunguza ushuru wa uingizaji wa mafuta nchini lengo likiwa kuifanya bidhaa hiyo isipande bei. Zoezi hilo lilianza mara moja na ndiyo iliifikisha bei ya Petroli kuwa Shilingi 3,000 kwa lita.

Hata hivyo, licha ya Serikali kutoa kiasi hicho cha pesa na bei ya mafuta kuwa Shilingi 3,000, bado bei ya bidhaa nchini ipo juu huku bei ya unga ikilalamikiwa kila kukicha kwamba, hadi Julai mwaka huu, kilo moja ya unga imefikia Tsh. 1,800 kutoka bei ya Tsh. 1,000 Februari mwaka huu.

Jana, Waziri wa Nishati, Januari Makamba alipotafutwa kwa njia ya simu ili kuulizwa kuhusu madai ya tenda kutolewa kwa uswahiba, hakupatikana hewani.
nini maoni yako?
nani apewe
 
Ubuyu kama ubuyu mwingine tu.
 
Back
Top Bottom