Gota8s
JF-Expert Member
- Aug 4, 2014
- 201
- 189
Habari za wakati huu wanajamvi:
Mimi sijambo kabisa naendelea vizuri, na naamini kila mmoja wenu anaendelea vema.. lakini ikiwa kjna changamoto yoyote kiafya nawaombea nafuu ya mapema.
Pasipo kupoteza muda mwingi nadhani niende mona kwa mona kwenye mada.
Hapa nitazungumzia zaidi jinsi gani masuala ya Teknolojia yanavyoathiri moja kwa moja ufikiri wa watoto na matokeo yake mpaka wanapokuwa watu wazima.
Binafsi sijakulia kwenye mazingira yaliyoendelea. Namaanisha kuwa masuala ya TV na Games za watoto hayakuwepo hata kidogo. Nilichokifanya ni ile michezo ya kawaida ya watoto inayochezwa vijijini. Kuwinda, kucheza mpira, kombolela na mingine kama hiyo.
Ila katika ukubwa wangu nimepata nafasi ya kuishi na watoto ambao ndio wanapitia sasa nyakati za kuishi maisha ya kiteknolojia.
Watoto wanaojua ratiba za vipindi mbalimbali vya televisheni kwenye king'amuzi chao, watoto wanaojua kufuatilia tamthiliya na katuni mbali mbali, watoto wajuzi wa kutumia vyombo mbalimbali kama simu, tablet, laptop n.k.
Watoto wa aina hii ndio ninaowazungumzia.
Waandaaji wa Games na Movie za watoto sijawahi kujua lengo lao ni nini. Kuna namna huwa nafikiri huenda kuna mtego wanaoutega.
Fiction inayotumika inakuwa imepita upeo na fantansy huwa zinawekwa hata pasipokuwa na ulazima.
Kwa mfano badala ya movie na games hizo kuwasaidia watoto kujifunza kutatua matatizo wanayokumbana nayo, utakuta heros wa movie hizo au games wanapata changamoto halafu purposeless wanapata magics na wana-overcome hayo matatizo.
Nimekuwa nikifuatilia sana katuni mbalimbali na nimegundua kuwa watoto huwa wanaishi ulimwengu tofauti na tunaoishi.
Watoto wanapewa imani kuwa siku zote watakutana na bahati kila watakapopata shida. Kwa mfano kuna katuni inaitwa Rango, hii inanisikitisha sana endapo baadhi ya watoto watachukua mafundisho yake na kuyajengea imani.
Despicable me, Frozen, cindelela, Grinch, home, ben10, son of Bigfoot, Rio n.k.
Pia zile movie za Spiderman huwajengea taswira watoto kushindwa kutatua changamoto zao wenyewe kwa kuamini mambo yale.
Kuna dogo wa miaka kama tisa hivi huwa muda mwingi nipo nae, akiagizwa kufuata kitu dukani ataanza kujisemea mwenyewe kuwa angekuwa Sonic angetumia sekunde tu akawa amerejea, au hata angekuwa spiderman angedanda kwenye majumba halafu arushe nyuzi zake achukue akitakacho kisha arudi haraka.
Pia waandaaji wa movie na game hizi wanawajaza ujinga watoto kuwa Bunduki huweza kutatua shida zao, yaani hata kitendo cha kuua mtu kwa bunduki watoto wanakichukulia kama jambo la burudani.
Watoto wanashindwa kuelewa kiundani thamani ya utu kwa kuwa ni suala la kawaida kumuona ninja kwenye movie akinyata na kuua watu na wakati mwingine kuwafyeka kwa mapanga. Baada ya hapo ninja huondoka kuendelea na mission.
Watoto hawawezi kujua inakuwaje mtu akifa au akikutwa popote amekufa process zinakuwaje, taratibu za kisheria na za kipolisi, uchungu wanaokuwa nao ndugu waliofiwa, uharamu wa tukio lenyewe la kuua.
Watoto wanawajua vema jinsi gani wa Vietnam wanavyokuwa wengi kwenye vita kisha wakipigwa risasi hata moja wanakufa nane
watoto wameshamezeshwa hizi propaganda za wamarekani juu ya ugaidi wa waarabu na dini yao ya uislam.
Watoto wameshaaminishwa na movie kama za Koi mil gaya (ya kihindi) kuwa hata asipofanya juhudi za kitaaluma kujiweka sawa.. atatokewa na miujiza (jadu) na atamgusa kichwa kisha atakuwa genious na strong.
Mimi huwa nafikiri kuwa kizazi hiki cha watoto walio under 12 kwa sasa, na uwepo wa simu, tv, computer, n.k basi kuna wakati utafika sisi tutakaokuwa wazee tutayatazama maisha magumu sana ya watoto wetu.
Hii nimeanza kuiona jinsi ilivyoathiri hata masuala ya mapenzi kwa kuwateka dada zetu. Wale akina dada wanaofuatilia tamthiliya za kifilipino, za kihindi na kikorea, huwa wanaamini zile fantasy za mapenzi ndio maisha yenyewe. Wanaamini inabidi wakutane na vijana wa kiume mahandsome
wenye sura laini wenye pesa zao kisha mapenzi yaende kwa mlolongo ule ule wanaouona kule.
Ndio maana hawa dada zetu walio wengi siku hizi kinachowakost ni kuwa mahusiano wanayoyatazamia kiuhalisia hawakutani nayo. Huishi wakiamini kuwa hawajampata mtu sahihi. Na akili inakuja kufunguka utu uzima ukishawafika.
Naamini wengi mna mengi ya kuongezea, kunirekebisha, kushauri au hata kuunga mkono.
Asanteni