Habari wana jf,
Mimi ni mdau mkubwa sana katika kufuatilia mambo ya elimu hapa nchini bila kujali ni mambo yanayohusu hatua ya chini niliokwishapita ama vinginevyo.
Ilikuwa kawaida kwa miaka ya nyuma kwa TCU kutoa kitabu kinachomuongoza mtu anayetaka kuomba kusoma fani mbalimbali vyuo vikuu mwezi wa nne mwishoni kuelekea wa tano. Hii ilikuwa inatoa nafasi ya kutosha kwa waombaji kusoma na kuzielewa program mbalimbali wanazozihita kuwa zinatolewa katika vyuo vipi. Hivyo kuwa na muda wa kutosha kufuatilia ubora wa vyuo watakavyoviomba kwa ajili ya program husika.
Kwa mwaka huu imekuwa tofauti. Mpaka sasa hakuna hicho kitabu online(yaani hiyo TCU guide book). Je, mnataka kukitoa wakati matokeo ya kidato cha sita yakiwa yametoka?
Sasa vijana waliomaliza kidato cha sita mwaka huu na wa nyuma yao ambao hawakuomba kudahiliwa kwa sababu mbalimbali wapo njia panda kwa tetesi wanazozisikia kuwa mwaka huu watakaodahiliwa vyuo vikuu ni wale wenye ufaulu wa daraja la 1&2 tu. Kama kijitabu hicho kingekuwepo tayari, wala uvumi huu usingewasumbua kwa sababu tayari wangekwisha kujua vigezo ni vipi kwa program mbalimbali. Je, mnasubiri muone ufaulu wa mwaka huu upo je ndiyo mtoke na kitabu chenu? Kwa maana serikali ya awamu hii haieleweki mnaogopa kutumbuliwa eti mmedahili vilaza?
Sisi hatujui yaliyowasibu majibu mnayajua nyinyi sisi kama jamii tunabaki na maswali. Awamu hii kila kitu kama kimesimama kinasubiri maelekezo kutoka juu.