Mlundikano wa Taasisi nyingi kwenye majukumu yanayokaribia kufanana ni upotevu wa pesa za umma kwa gharama za pango, magari, posho za wajumbe wa bodi na vikao vingi visivyo na tija.
PENDEKEZO: Iundwe BODI YA ELIMU YA JUU, Higher Education Council, HEC (ikiwa na Idara za UDAHILI/Kuboresha Ubora wa Elimu - Quality Assurance, utoaji/urudishaji MIKOPO). Wafanyakazi wengine wapunguzwe kwa kupewa stahiki zao zote.
NB: Ni aibu taasisi kama hizi tena baadhi zinaongozwa na Maprofesa (PhD) kukosa ufanisi wa kudahili wanafunzi wasio na sifa, pia baadhi ya vyuo vikuu binafsi utoaji wa elimu huko ni wa kutiliwa shaka sana, mnasubiri nini kuvifuta? Wasomi mnatuangusha jamani.