kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 13,506
- 13,988
TCU hongereni sana kwa jitihada za kusimamia utoaji wa taaluma na uendeshaji wa vyuo vikuu nchini. Kwavyovyote vile kazi yenu sio ndogo. Hongereni sana pia kwa kutoa miongozo mbalimbali ya taratibu za namna ya kuendesha na kufanikisha mambo mabalimbali kwenye elimu ya juu.
Angalizo tu ni namna ya ushirikishwaji wa wadau katika masuala yanaoyoathiri mafunzo ya taaluma (professions) mbalimbali ambazo ziko chini ya TCU.
Mfano, kuna kila dalili kuwa TCU inawashirikisha zaidi Madakitari (Medicine) kwenye maswala yanayohusu mafunzo ya taaluma za Afya (Health and Allied Sciences) kwenye kupata maoni na kufanya maamuzi kuliko taaluma nyingine za Afya kama vile za pharmacy, Laboratory, Nursing, Radiology, nk. Hivyo, TCU inapata maoni na kufanyia kazi matakwa ya upande mmoja wa Medicine zaidi kuliko matawi mengine ya Afya.
Inafahamika kuwa Medicine ni taaluma ya zamani sana ambayo imepata mafanikio makubwa sana nchini na duniani, hivyo ina wasomi wengi sana wa viwango mbalimbali kuanzia certificate, diploma, bachelor, MMed, PhD na ina maprofessor na associate professors wengi sana nchini. Hivyo, kuwapata viongozi ambao wana PhD na maprofessor kwenye uongozi wa Medicine ni kazi ndogo sana, maana wapo wengi kwenye jamii kuliko kwenye Pharmacy, Laboratory, Nursing, Radiology, Nutrition, ect. Professions nyingine za Afya ndiyo kwanza zinafanya capacity building kwa wanataaluma wao, PhD/Masters holders ni wachache sana.
Ukurasa wa 24 wa Handbook for Standards & Guidelines for Universities Education in Tanzania (STANDARD 1.2: Management Structures), guideline number 1.2.5 inaonyesha ukweli huu kuwa TCU inapokea maoni kutoka watu wa Medicine kuliko watu wa taaluma nyingine za Afya. Kwanini ni watu wenye master degree (MMed/MDent) tu waruhusiwe kushika nafasi za uongozi lakini watu wenye Master kwenye taaluma nyingine za Afya wasiruhusiwe kushika nafasi equivalent kwenye vyuo vyao wakati wote wana respective Master degree za taaluma zao?. Na ukizingatia kuwa hizi taaluma nyingine za Afya hazina wasomi wengi kama ilivyo kwa Medicine. Mimi nilidhani kinyume chake ndio ingekuwa sahihi. Hakuna ubishi kuwa hii haikutokea kwa bahati mbaya Wala kuwa na scientific justification, bali Kulikuwa tu na shinikizo kubwa kutoka Medicine na ukosefu wa wawakikishi kutoka vitivo vingine vya science za afya.
Entry qualifications: TCU pia inahangaika zaidi na entry qualifications za wanafunzi wa Medicine kuliko wa taaluma nyingine za Afya.
Harmonization of Curricula: Hapa pia TCU inaonyesha wazi kuwa haina habari na taaluma nyingine za Afya.
Hii ni mifano tu ya dhambi wanayoifanya TCU kwa fani nyingine za Afya kwenye Elimu ya Juu.
Labda nitoe ushauri wa wazi kwa chombo chetu hiki muhimu nchini kuwa, ni lazima taaluma zote vyuo vikuu zipate uwakilishi wa kutosha, yaani wapate wawakilishi kutoka kwenye schools/vitivo vya sayansi za Afya vyuoni badala ya kuita uongozi wa Vyuo. Mara nyingi Vice Chancellors na Manaibu wao kwenye vyuo vya Afya ni kutoka Medicine, hivyo wanasema zaidi ya kitivo cha medicine zaidi kuliko ya vitivo vingine.
Ni maoni tu.