TCRA wana magical button ya kuswitch off simu zote feki au tunapeana presha tu?

Michael Ngusa

JF-Expert Member
Aug 4, 2014
1,637
458
Wadau,
Hawa watu wanasema ifikapo June watazima simu zote feki, ajabu washalamba ushuru wa simu hizo na wao wenyewe (serikali) ndio waliotoa kibali ziingie nchini na kuuzwa. Anyway, swali langu ni dogo tu, je, TCRA wana magical button ya kuswitch off simu zote feki? how do they control our phone countrywide? Ningependa kufahamu the technology behind. Isije kuwa mbwembwe tu.

 
Makampuni ya cm yatakuwa yana tuma product na IMEI namba kwenye system yaani kila kampuni ya kuzalisha sim inalink mfumo wa ysajili wake wa imei namba na mtambo Wa TCRA hivyo TCRA watazitambua simu kupitia imei kutoka kwa wazalishaji wanao tambulika kwa kwa viwango na TCRA TU.
Ni rahisi tu.
 
Kwa haya maelezo, ni kwamba TCRA ndo walikua na uwezo wa kujua simu feki na kuzizuia kuingia sokoni. Hili kosa ni lao sasa kwa nini waadhibiwe wengine?
 
Hiyo ni hypothesis yako au ni fact?
Kitu unachokizungumzia hapa ni kigumu sana kuliko unavyodhania. Siyo rahisi manufacturers (there are lots, lots of them) wawasilishe IMEI numbers kwa TCRA kwa sababu hawana sababu ya kufanya hivyo na hakuna sheria inayowalazimisha kufanya hivyo. Chukulia kwa mfano Apple, hawauzi kabisa (Yes, hawauzi) simu Tanzania, uwaambie Apple Inc. wawasilishe IMEI za simu zao zote TCRA itakuwa kichekesho! Lakini eventually iPhone zinaingia Tanzania, na hauwezi kuzizuiya zisiingie!! Wenye uwezo wa kublock IMEI ya simu isipate mawasiliano ni carrier, lakini kwa simu hizi za mchina carrier ni ngumu kujua simu fake na halali kupitia IMEI peke yake. Simu nyingi "fake" au clone zinamajina ya kwa juu tu, lakini IMEI zake ziko associated na identity zake halali, yaani jina la board!

Sijuwi ni uvivu wa kufikiria tu au kukwepa majukumu, lakini anayetakiwa hasa kudhibiti simu clone, na simu zilizo chini ya viwango siyo TCRA, ni TBS. TBS ndiyo wenye dhamana ya kuhakiki viwango vya bidhaa zote zinazotengenezwa na zinazoingizwa ndani ja JMT. Ukikutana na vitasa, redio, televisheni, fenicha, simu, au kitu chochote kimeingizwa nchini na kinauzwa sokoni wa kulaumiwa na TBS. Huwezi kuanza kupiga hodi nyumba kwa nyumba kutafuta viti "fake" na kuvikamata kwenda kuvichoma moto, mlaji wa mwisho amekikuta tu sokoni, akaona bei nafuu akanunua, ukimuuzia lawama wakati wewe umeshindwa kutimiza wajibu ni ufinyu wa fikra usiomithilika!
 

Mkuu umemaliza kila kitu hapo. Ndio maana nasisitiza wahusika waache kukurupuka.
 
kamwe hawatazima! wakifanya hivyo nitawaburuza mahakamani kwa niaba ya wananchi walala hoi! vinginevyo zoezi hili lifanywe kwa expenses za madhibiti wa ubora wa bidhaa zinazoingizwa nchini! hebu fikiri ingekuwa ni dawa au chakula kuwe fake wangapi tungewazika!!? No! they have to rethink!! hapa cha msingi si ku restart bali ni kuanza from now kudhibiti zinazoingia! mbina. Mbona noti za zamani zimeachwa zife kifo cha kawaida na imewezekana? why not fake phones!!
kweli nitapinga on behalf of innocent people!
 

Naona Umeongea pointi. Kama manufacturer ndiye ana jukumu la kutuma IMEI kwa TCRA ina maana awasilishe IMEI za simu zote alizotengeneza bila kujali kama simu zingine hazikuletwa na kuuzwa Tanzania (yaani hata zile ambazo zimeuzwa mataifa mengine), kitu ambacho si rahisi na pia si kisheria.

Now, is it possibe for us to muster up our courage and do something to get rid of all this nonsense?

Au tuendelee kuamini kuwa zoezi halitekelezeki na kuumiza low income earners wenye shaka ya kuzimiwa simu zao.
 
Sure, ignore TCRA na kitisho chao kisicho na mashiko!
 
Nadhani Zile hela za fidia ambazo wangepaswa kuwalipa wananchi
Wao,
WATAWALIPA makampuni ya simu ili Wawafanyie kazi ya kuwatumia IMEI zetu...
ITS NOT FAIR AT ALL
 
Wakuu nilikuwa naangaria simu yangu kama ni original lakin ilichoniletea si kutegemea imesema simu hiyo HAIPO eti niwasiliane na MTU aliyeniuzia kabla ya mwezi Wa sita.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…