TCRA wamulikeni Halotel, simu feki iliyozimwa yafanya kazi kwa line ya Halotel

Mwabhleja

JF-Expert Member
Jan 27, 2016
1,351
2,061
Siku chache zilizopita mamlaka ya mawasiliano Tanzania (TCRA) wametangaza kuwa wamezima namba tambulishi (IMEI) 603,000 sawa na asilimia 2.9 ya vifaa vya mawasiliano ikiwa ni pamoja na simu feki zinazotumika nchini.

Kuzimwa kwa vifaa hivyo ni utekelezaji wa agizo la serikali la kuondoa bidhaa feki za mawasiliano kuanzia Juni 2016.

Ofisa Uhusiano wa TCRA, Innocent Mungy, alisema vifaa vya mawasiliano vilivyozimwa ni pamoja na simu za mkononi, ipad, tableti na modemu.

Katika hali inayothibitisha kuwepo kwa aidha hujuma au udhaifu wa kimtandao katika uzimaji wa simu feki, mtu mmoja ambaye mkoani Geita ameripotiwa kutiumia simu yake feki licha ya kwamba awali ilikuwa imezimwa.

Usiku wa uzimaji simu, alikuwa ameweka line ya tigo na voda na simu yake ilizimwa mpaka sasa haifanyi kazi kwa line zote isipokuwa kupitia line ya halotel.

Katika kusimamia maamuzi ya serikali kupitia TCRA, ni wakati wa kuchunguza zaidi kuhusiana na jambo hili kusudi taratibu zote zifuatwe na ikibidi simu zote zilizo feki zizimwe.
 
Kifupi tuseme TCRA wamefeli kwa hili, kama Holatel wameweza basi mtu yoyote anaweza kufanya uhuni huo na hatimaye ikaonekana ni ghiriba tu.

Vita vya teknolojia vinahitaji ubunifu wa hali ya juu sana.
 
Sio kweli,mm nina line ya halotel na simu ilizimwa tarehe 17 saa nne asb na mpk leo haijawaka ingawa ina line hiyo ndani.
 
Zimezimwa IMEI laki 6+ lakini simu zinaweza zisiwe zaidi ya laki moja..
 
Kweli ww ni mnoko! Kinakuuma kuona jamaa yuko hewani! Yaani baadhi ya wa tz mnanishangaza sana, mna ka hali ka kuona bora mkose wote kuliko mwengine kupata! Yaani bora wote muwe maskini kuliko kuona wachache wananeemeka! (Nadhani huo msemo mmenielewa sina haja kudadavua!) No wonder!
 
Kwa hiyo unakomalia matumizi ya simu feki, je unajua ni kitu gani kitafuata au akili yako inawaza kwamba kila mmoja na roho ya wivu. Inaweza isiwe wote but coincidentally imetokea, siku zijazo kuna kesi nyingi zinakuja za watu kuflash simu na kubadili IMEI number lengo la huu uzi ni kuhakikisha Mtanzania hashitakiwi kwa kosa ambalo si lake. Sikuwahi kuzimiwa simu na simu zangu zote ziko hewani, try to think positively
 
Hiyo mbona ni kwa line zote wakizima Halotel unaweka airtel inafanya kazi hivyo hivyo line zingine.
 
Sio kweli,mm nina line ya halotel na simu ilizimwa tarehe 17 saa nne asb na mpk leo haijawaka ingawa ina line hiyo ndani.
No research mo right to talk, unapoambiwa wenye vipara wengi wana akili haimaanishi kwamba wote hivyo jambo hili limetokea kweli ni vema tahadhari zikatolewa ili mtu asijekushitakiwa kwa kosa la mamlaka. Mpaka sasa laini iliyokuwemo wakati simu zikizimwa haisomi but ile ya halotel inasoma.
Tatizo la Watanzania tunatanguliza hisia zetu mbele badala ya kujifunza kama jambo hilo linawezekana au haliwezekani. Hujiulizi ni kwanini mafundi simu wanapigwa mkwara mzito if the system can control everything?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…