TCRA Ondoeni kwenye orodha namba tunazofuta

Molaro

JF-Expert Member
Nov 9, 2013
818
577
Habari wamajambi na TCRA

Nimefuta namba 4 zilizosajiliwa kwa NIN yangu zaidi ya miezi 6 iliyopita ila ajabu ni kwamba bado hizo namba zipo kwenye orodha ya namba zangu nikiangalia kwenye orodha ya namba zilizosajiliwa kwa mitandao yote.

Pia nikiangalia kwa Mobile money (M pesa/tigo pesa) namba ya TTCL bado inasoma kwa majina yangu pamoja na kuifuta zaidi ya miezi 6 sasa. Ni vyema mngeondoa namba zote ambazo zinafutwa na sisi wateja ili hata mtu anaposajili namba kwa vitambuliso vyetu tuweze kugundua mapema badala ya kuwa na orodha ndefu ya namba usizozitumia wala kuzitambua.

Sambamba na hilo naomba mrudishe huduma ya Mobile Number Portability (MPN) ili tuepuke kuwa na mzigo wa line za simu. Unaweza kutoka eneo X ambalo Mtandao A upo vizuri ukahamia eneo Y na huko unakuta mtandao B ndio unafanya kazi vizuri, sasa badala ya kusajili namba nyingine ya mtandao unaofanya vizuri huko bhasi ungehamia mtandao husika bila kulazimika kubadili namba.

Naamini mtafanyia kazi maoni hayo
 
Back
Top Bottom