TCRA, kaeni na RFA na Clouds FM, kwanini mtangazo huwa yanakatika zaidi ya mara tatu kwa saa moja?

nyumbamungu

JF-Expert Member
Mar 3, 2017
1,032
893
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania "TCRA" pamoja na kusimamia mawasiliano, pia ni mamlaka ya Udhiti kwa upande wa mawasiliano, yakiwemo masafa ya redio.

Naomba nijikite kwenye redio, najuwa upo mchakato kuanzia kuandaa, kurusha, hadi kumfikia msikilizaji iwe ni matangazo ya redio au televisheni.

Hivyo kwa mamlaka mlio nayo kama ilivyo LATRA, mnao uwezo wa kuwaandikia barua Redio Free Afrika na Clouds Fm kuwa uliza kwanini inakuwa kero kwa wasilikizaji kukatikakatika kwa matangazo, tena ingekuwa inajitokeza angalau mara moja kwa wiki ingawa sio rasmi, kuliko ilivyosasa.

Na nyie wamiliki wa hizo redio RFA na Clouds FM, tunawaomba mfanye marekebisho ya mitambo yenu ili msiwe kero kwa wasilikizaji wenu na wateja wenu wanaowapa matangazo..

Yote kwa yote RFA mumezidi kupindi magazeti 12:30 asubuhi matangazo yamekatika kwa zaidi ya mara 6 wakati kipindi chenyewe kina dakika 20 za kusoma magazeti, hata mnapojiunga na BBC, DW na VOA huko ndio usikivu unashida sana.
 
Back
Top Bottom