Shagiguku
JF-Expert Member
- Jan 9, 2010
- 407
- 133
Hello wananzengo wa Tanzania popote mlipo duniani. Nautupia huu uzi humu ili tuujadili kwa pamoja.
Kumeibuka wimbi la "Mikate ya Maziwa" hapa nchini. Kila sehemu ipo inauzwa.
Maswali yangu machache kwa mamlaka za udhibiti ubora (TMDA na TBS) ni haya:
1. Je, tuna taarifa za kutosha juu ya ukweli wa uwemo wa maziwa kwenye mikate hiyo? Ama wananzengo tunalishwa kemikali za kichina nanyi mkiwepo kama wapenzi watazamaji!
2. Baadhi ya wazalishaji wa mikate hiyo ya maziwa wanatumia hadi logo yenu kwenye vifungashio vyao kuonesha kwamba wamethibitishwa na ninyi. Je, ni kweli mmewathibitishia ubora wa mikate hii?
3. Je, ni kweli kwamba mwananzengo mimi leo nikisema niende kwenye kiwanda kimojawapo cha uzalidhaji wa mikate ya maziwa nitayakuta hayo maziwa ya kweli yapo kwenye ma-container ya kuhifadhia yakisubiri kutumika kutengenezamikate hiyo?
4. Na kama yapo hayo maziwa ya ukweli, je, mamlaka zetu za udhibiti (TMDA na TBS) mmejiridhisha kuwa ni maziwa ya mnyama gani?
5. Je, huku mtaaani kuna mwananzengo yeyote anaye-supply maziwa ya ukweli kwa hawa wazalishaji wa mikate ya maziwa angalau atuthibitishie kuwa ni kweli huwa anapeleka maziwa ya ukweli kwa mmoja wa wazalishaji mikate ya maziwa ili kututoa wasiwasi?