benzemah
JF-Expert Member
- Nov 19, 2014
- 1,533
- 3,186
Kufuatia lile kongamano aliloshiriki Harrison Mwakyembe ambapo mmoja wa wazungumzaji alieleza uwepo wa dawa za meno na "body spray" zinazoongeza homoni za kike kwa wanaume. shirika la viwango Tanzania (TBS) limetoa tamko kukanusha madai hayo huku ikieleza inaendelea kufuatilia
JISOMEE HAPO CHINI
Dar es Salaam, 01 Aprili, 2023
"Hivi karibuni, kumekuwepo na taarifa inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii inayoelezea uwepo wa dawa za meno zinazotolewa kama msaada katika baadhi ya shule hapa nchini zinazosadikika kuwa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) tumepima na kuthibitisha zina viambata ambavyo ni vichocheo vya kibiolojia (hormones) vinavyoathiri watumiaji hasa watoto wa klume.
TBS inakanusha maelezo ya kwenye ujumbe wa maneno unaosambaa kwenye mitandao ya kijamii kuwa ilipima bidhaa hizo za dawa za meno na kutoa taarifa kuwa zina vichocheo hivyo vya kibiolojia.
Aidha, TBS baada ya kupata taarifa hiyo imefanya ukaguzi na uchunguzi wa awali katika bidhaa husika na kugundua hakuna uwepo wa vichocheo hivyo vya kibiolojia
Hata hivyo TBS inaendelea kufanya ufuatiliaji wa suala hili kwa kushirikiana na maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali.
TBS inawashukuru wananchi wote ambao wanaendelea kutoa ushirikiano kwani suala la udhibiti wa usalama na ubora wa bidhaa ni mtambuka (shared responsibility).