TBC YAJA NA KIPINDI KIPYA CHA MADA KUU

Jul 8, 2013
53
75
Shirika la Utangazaji Tanzania TBC kupitia luninga ya Taifa TBC 1 limeanzisha kipindi kipya Kiitwacho “MADA KUU”.

Ni kipindi kinachohusu mijadala moto moto kuhusu masuala mbalimbali yanayojiri katika jamii iwe ni siasa, uchumi, michezo, uongozi n.k

Tayari TBC imejizolea umaarufu miongoni mwa watanzania kupitia vipindi mahiri vinavyoelemisha na kuchochea uwajibikaji.

Kipindi cha Mada Kuu kitakuwa kinaruka kila Alhamisi saa 11 hadi saa 12:30 jioni.

Watangazaji wa Kipindi hiki ni Flora Mwano, Esero Mafuru, Fredrick Nwaka na Maulid Kambaya.

Karibu kufuatilia kipindi hiki na kuwa sehemu ya mijadala muhimu ya kitaifa.
953eabf3-bc3f-4f9a-84ee-86063b094d77.jpeg
 
Waendeshaji wa kipindi hicho wana uvumilivu juu ya mambo ambayo serikali huwa haitaki kusikia?
Mfano:Kwanini serikali haijawahi kupeleleza tukio la jaribio la mauaji lililotaka kuondoa uhai wa Tundu Lissu?
Kama waendeshaji wa kipindi hicho wanao uvumilivu huo basi kinastahili kuitwa hivyo,lakini kama hawawezi kuvumilia mambo kama hayo wavadirishe jina la kipindi
 
Kipindi pekee nilikuwa naangalia TBC ni mchakato majimboni, hiyo ni mwaka 2010. ULIMWENGU WA KISWAHILI cha Suleiman Hega, Pia This week in perspective cha Adam Simbeye. Sijui kama bado kipo
 
Maulid kammbaya huyuhyu asiye na busara aliyekua malumbano ya hoja..........

*NJE ya mada kidogo:-
*Mtangazaji wenu sijui MIKITO ni muhuni na ni gangwe....kipindi cha saa kumi alfajiri wenzake wanaruhusu tuchague wimbo uwasindikize watu walau watatu yeye hataki.
*Ana manyimbo ya bongo fleva anadhani sisi wote ni wahuni.
****
*MWINGINE NAKAZIA KABISA....anaitwa WARUNGU....namba sana muwafikishie viongozi huko kuwa sisi wasikilizaji wastaarabu HATUMTAKI....kwanza WAMEUA RADIO YAO HUKO haikusikilizwa kwa mambo ya USHAMBA....Sasa mmemleta huku muda wote ni KUJISIFIA TU NA MA-JINGLE ya WAJALUO.....ANABOA tena mmemuongezea muda mpaka saa 6....mna KICHAA sio bure.....mnaacha kuwaweka kina MASOUD MASOUD tuelimike mnamuweka TAKATAKA WARUNGU...HAYO MATUZO YAKE YA BEST NASO ASITUSUMBUE SISI wakati wa kulala..tunatafakari maisha unasikia "baba mzazi warungu wachape"..

HUWA NAHAMIA RADIO ONE KWA ZOMBOKO mpaka amalize PINDI LAKE.

***KINGINE....ni kipindi cha MAHUSIANO NI KIPINDI KIBAYA KINAVUNJA NDOA....MADOKTA WANAZUNGUMZIA UHALALI WA WAKE KUCHEPUKA.....NI KIPINDI CHA KIPUMBAVU.

HIYO NI KERO YANGU...SINA CHUKI.
 
Back
Top Bottom