Sanyambila
JF-Expert Member
- Jan 24, 2018
- 368
- 501
Habari wadau wa michezo,
Kuna tetesi au taarifa ya kweli ikihusu TBC1 kuonyesha mechi za Kombe la Dunia nchini Qatar mechi takribani 28 ni jambo la kupongezwa sana.
TV'S Kama KBC, UBC, MBC YA Malawi hizo TV's kila Kombe la Dunia wanaonesha ila TBC tu ndiyo huwa wana tuweka gizani, hata mechi za Taifa Stars zilikuwa hazionyeshwi na TBC. Sasa World Cup Broadcasting Rights inataka televisheni za taifa tu ndiyo wawe kipaumbele kurusha mitanange hiyo. Sasa hapa TBC msilale, ndiyo maana hata Azam TV wamekosa haki ya kurusha matangazo hayo.
Kama habari hizi ni kweli kongole saana kwenu TBC ila kama ni uvumi tu mtakuwa hamjatutendea haki Watanzania, maana mnahisi sisi tunataka muonyeshe mambo ya siasa tu!
Hapana hata burudani mzipe kipaumbele kama mipira, ndondi, riadha, ikiwa tu ni timu yoyote ya taifa inacheza onyesheni. Kuna maana gani ya kuwa chombo cha taifa halafu kimejikita zaidi kwenye ziara za Rais, Mawaziri, Bunge ila siyo burudani pendwa kama mipira?
Kila l aheri, TBC1 Ukweli na Uhakika.⚘⚘⚽️⚽️⚽️🏆🏆🏆