KERO  Tatizo sugu la Maji jijini Mwanza

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Wadau,

Mwanza ni Jiji kubwa kwa wingi wa watu na rasmilimali lakini linakubwa na tatizo sugu na kubwa la mgao wa maji ambao haueleweki.

Mfano: Nyegezi maji kwa wiki baadhi ya mitaa wanapata mchana maramoja kwa wiki au wanatolewa usiku wa manane! Mradi mkubwa wa maji unaotekelezwa (Butimba) ulisemekana kuwa utakuwa suluhu ya tatizo la maji ambapo ulizidiuliwa na kuanza majaribio mwaka Jana (December) lakini tatizo halijatatulika.

Mathalani, Titizo hili la maji lilimuondoa Hadi aliyekuwa Mkuu wa Idara ya maji Mwanza mwaka Jana!

Swali langu: Je, ni sahihi watu (masika na kiangazi) kuendelea kuteseka na shida ya maji hapa Mwanza?

Watendaji wa idara ya maji Mwanza mnalipwa kwa Kodi zetu, tafadhari timizeni wajibu wenu. Kama nafasi haziwatoshi, mtaarifuni Waziri alete watu sahihi wa kuishughulikia tatizo hili! Msikae kwenye nafasi ambazo hamtoshi kuzitendea haki!

Maji ni uhai .. maji sio Anasa

Naomba kuwasilisha

Ufafanuzi wa MWAUWASA ~ MWAUWASA: Mwanza hakuna changamoto ya uhaba wa huduma ya maji, mteja mwenye changamoto awasiliane nasi
 
Wasukuma mna akili au vichwa mnafugia nywele.
Ziwa liko hapo zero distance Tena hayo maji hayahitaji desalination Kama kule Gaza, halafu mnakuja kwetu Dodoma kulalamika eti hamna maji.
Madiwani mnao, Kodi mnatoza,
Wabunge mnao, wakuu wawilaya mnao na wakurugenzi mnao.
Tumieni hao wasanii mlionao waende Somalia kuomba msaada wa fedha na mainjinia waje wawaleteeni maji toka Musoma.
 
Pale Kigongo ferry ziwani kabsa na hawana maji, 😆😆😆😆nacheka kwa huzuni
Halafu waarabu wa jangwani Dubai wakipewa mkataba wa kuja kuendeleza misitu huku kwetu tusiwe tunalalamika. We can't do shit! Yaani sisi mbali na ufisadi hatuwezi kufanya cho chote kwa ufanisi na weledi. None! Zero! Nada! 🚮🚮🚮🚮
 
Mwanza maji yapo,suala ni wewe unaishi wapi,kule Capri Point maji na umeme havikatiki. Lakini inasikitisha sana,ziwa lipo hapo shida ya maji inatoka wapi? Lakini ni heri nyie Mwanza,nenda Butiama Ziwa liko jirani lakini huu mwaka tangu January hadi May maji yametoka mara 3 tu,watu wako ofisini kila siku na mishahara wanapata.
 
Huna ndoo mkuu? Shuka ziwani rudi geto yatumie maji uliyochota
 
Back
Top Bottom