Jana Rais Magufuli akiongea na Wazee wa Dar es Salaam, katika mambo mengi ya msingi aliyogusia na kusisitiza ni ufisadi. Kwamba nchi hii ni tajiri lakini watu wachache ndio WAMEIFIKISHA NCHI hapa ilipo (omba omba).
Yawezekana ni kweli lakini uhalisia ni kwamba kumekuwa na uzembe katika usimamizi wa shughuli serikalini na Taasisi zake. Hili linaweza kupimwa kwa viashiria/vigezo vifuatavyo:
(1) Ubora wa huduma za umma.
(2) Ubora wa utumishi wa umma na uhuru wake kutoka kwenye shinikizo la kisiasa.
(3) Ubora wa uundaji na utekelezaji wa sera, na
(4) Uaminifu na dhamira ya serikali kutekeleza sera zake.
Wananchi kwa sasa wana matumaini makubwa na Serikali ya Magufuli kwamba itasimamia, kwa nguvu zake zote, kufikia vigezo vinne hapo juu.
KUPANGA NI KUCHAGUA WAKATI NDIO HUU.